
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akizungumza wakati akiifungua semina ya Wahariri Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu mafao mbalimbali katika mifuko ya hifadhi ya jamii, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji (SSRA), Sarah Kibonde Msika.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (wa tatu kulia), akiwa kwenye semina hiyo. Kulia ni Mjumbe wa bodi ya Jukwaa la Wahariri na Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Nevil Meena na kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Irene Isaka, ili kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika semina hiyo.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakifuatilia mada katika semina hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (aliyesimama), akizungumza na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Nevil Meena (kulia). Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.

Baadhi ya wahariri wakinukuu baadhi ya maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika semina hiyo.

Juu na chini: Ni baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari, wakifuatilia semina hiyo.
![]() | ||
|






No comments:
Post a Comment