TANGAZO


Tuesday, September 20, 2016

Makao makuu ya upinzani yachomwa DRC

Afisi ya chama cha upinzani iliochomwa moto

Image captionAfisi ya chama cha upinzani iliochomwa moto
Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yamechomwa moto katika mji mkuu wa Kinshasa huku mili miwili ilioungua ikipatikana ndani yake.
Mashambulio hayo yanajiri kufuatia makabiliano ya siku ya Jumatatu kati ya maafisa wa polisi na wafuasi wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu ifikiapo mwezi Disemba.
Maandamano nchini DRC
Image captionMaandamano nchini DRC
Ofisi ya chama kikuu cha upinzani UPDS ni miongoni mwa zile zilizochomwa mjini Kinshasa.
Upinzani umemuonya Kabila kwamba atakuwa akifanya ''uhaini'' kwa kuchelewesha uchaguzi.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba ,lakini upinzani unahofia kwamba rais anataka kuuahirisha kwa lengo la kutaka kusalia madarakani.
Bado hajatoa tamko kuhusu mipango hiyo.

No comments:

Post a Comment