Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kuagwa kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya kuagwa kwa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo leo Jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipongezwa na mototo wake wa kike, Bi. Noera Kileo wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu, leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (watatu kutoka kushoto)akiwa katika
picha ya pamoja na Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo
(kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia
takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
Na Sheila Simba-Maelezo
MAHAKAMA nchini zimetakiwa
kuzingatia haki ya msingi katika kutenda kazi,kuliko ufundi wa kisheria unaotumiwa
na wanasheria katika kufanya kazi zao za kila siku.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es
Salaam na Jaji Angera Kileo katika hotuba yake wakati wa hafla ya kumuanga
iliyofanyika katika ofisi za Mahakama Kuu.
Amesema kuwa ni vyema haki
itendeke kwa kila mtu ili kusaidia jamii kupata haki pale wanapokua na tatizo
na kuongeza kuwa ni imani yake kuwa mwenye mamlaka ya kutoa uhai ni yule
alikupa uhai pekee.
“Watoaji haki sio wote
wamekamilika tunapoamua kutoa hukumu ya kifo unaweza kutoa kwa mtu ambaye
hakutenda kosa hilo na kumuacha aliyefanya kosa”alisema Jaji Kileo
Aidha,ameeleza kuwa mahakama zinahitaji
kusaidiwa katika kazi zake za uendeshaji wa kesi kwani ni gharama na wakati
mwingine mahakama zinashindwa kutimiza wajibu wake kutokana na kushindwa kumudu
gharama.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa
Tanzania Mohamed Othmani Chande, akizungumzia wasifu Jaji Kileo amesema mahakama uadilifu na
uaminifu wa Jaji huyo katika kipindi cha miaka 40 aliyoitumia sekta ya sheria
nchini.
“kwa kweli Jaji Kileo amefanya
kazi kubwa na anaondoka akiwa ametuachia urithi mzuri hasa wa kutumikia haki ya
msingi katika kutenda haki na sio kuangalia ufundi wa kisheria kama ambavyo
alivyokuwa anafanya kazi” alisema Chande.
Ameongeza kuwa Jaji Kileo
alikuwa ni mtu wa kuhakikisha kila mtu
anapata haki yake na kuheshimu haki na kusiitiza majaji wanawake kuiga mfano
wake ili kusaidia mahakama kufanya kazi zake kwa kuzingatia maadili ya kazi.







No comments:
Post a Comment