TANGAZO


Thursday, September 15, 2016

Choo kilichotengezwa kwa dhahabu kutumika na umma

Choo kilichotengezwa na dhahabu

Image captionChoo kilichotengezwa na dhahabu
Raia wako huru kutumia fedha zao kidogo ili kupata huduma ya choo kilichotengezwa na dhahabu katika jumba la makumbusho la Guggenheim.
Msanii kutoka Italy, Maurizio Cattelan alijenga choo hicho kwa kutumia carat 18 za dhahabu na kukiita choo hicho Marekani.
Choo hicho cha maonyesho kimewekwa katika msala wa kuogea wa Guggenheim kulingana na the New Yorker.
Msanii Maurizo Cattelan kutoka Italy
Image captionMsanii Maurizo Cattelan kutoka Italy
Jumba hilo la makumbusho limekitaja choo hicho kuwa kazi nzuri.
Choo hicho cha dhahabu kilijengwa katika choo chengine kinachotumiwa na jinsia zote mbili.
Wageni wanaolipa kiingilio cha jumba hilo la makumbusho wataweza kukitumia wanavyotaka.
Choo kilichotengezwa na dhahabuImage copyrightTWITTER
Image captionChoo kilichotengezwa na dhahabu
Choo hicho kinalenga kuwapa fursa raia wa tabaka la chini kujifurahisha katika mandhari ambayo hutumiwa na matajiri pekee.

No comments:

Post a Comment