TANGAZO


Thursday, August 11, 2016

"WATANZANIA ZAIDI YA 1000 WANUFAIKA NA MAFUNZO NCHINI JAPANI"

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo. 
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu YOSHIDA akizungumza katika afla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi (12)waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (03), mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo. 
Watumishi (12) waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (waliosimama) wakijitambulisha mbele ya  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ( wa pili kulia mstari wa mbele) na Waandishi wa Habari (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo. 
Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto)  akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo. 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kulia mstari wa mbele) akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto)  wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.

MAHUSIANO yaliyodumu kwa muda mrefu  baina ya Serikali ya  Tanzania na  Japani yamewezesha watanzania  zaidi ya 1000   kupata mafunzo  katika vyuo  mbalimbali  nchini Japani  kwa kipindi cha miaka 8  ambayo yamesaidia kuwa na rasilimaliwatu yenye tija katika maendeleo ya kiuchumi  nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menentimenti  ya Utumishi wa Umma,  Dkt. Laurean Ndumbaro kwenye hafla fupi ya kuwaaga  watanzania 12 waliopata fursa   ya mafunzo  ya Shahada ya Uzamili nchini Japani  kwa ufadhili  Serikali ya Japani  kupitia   Mpango wa  ABE  initiative, iliyofanyika  leo nyumbani kwa balozi wa Japani nchini  Tanzania .

 “ Kati ya mwaka 2008 hadi  2015 zaidi ya watanzania  1000 wamepata mafunzo  katika vyuo mbalimbali nchini  Japani  kupitia ufadhili wa Shirika  la kimataifa  la Maendeleo la Japani ( JICA)  na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika  kuwajengea uwezo  watumishi wa umma na watumishi walio katika sekta binafsi” alisema Dkt.  Laurean Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro  alifafanua kuwa,    Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendelo  la Japani  limewawezesha vijana  wengi wa kitanzania   kupata mafunzo  ya shahada  ya Uzamili kupitia  Mpango wa  ABE  initiative,ambao    baada ya  kumaliza mafunzo , wanarudi  nchini   Tanzania  na kuanza kujenga  ushirikiano  wa kibiashara  kati ya  Tanzania  na Japani  na pia  kuchangia  katika maendeleo ya sekta  ya viwanda  nchini”  alisisitiza Dkt. Ndumbaro.

 “ Katika  awamu ya kwanza mwaka 2014  walienda vijana  29  na awamu ya pili  ambayo ni mwaka  2015 walienda  vijana 32 kwa ajiri ya kupata mafunzo nchini Japani, ambapo mpaka sasa idadi ya wanufaika wa mafunzo hayo imefikia 73” alifafanua Dkt. Ndumbaro.

Aidha Dkt. Ndumbaro  aliwataka  vijana waliopata fursa ya mafunzo hayo nchini Japani  kusoma kwa bidii  na kutumia elimu na ujuzi watakaoupata kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

Alisema,  ushirikiano baina ya Serikali ya  Tanzania  na Japani   umeanza tangu mwaka 1960  ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania ilipata fursa ya kupeleka  watanzania nchini Japani mwaka 1962 kwa ajili ya kupata mafunzo  katika vyuo mbali mbali nchini humo.

Kwa  upande wake  Balozi wa Japani nchini  Mhe. Masaharu Yoshida alisema, Japan itaendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchi hizo mbili ili kila upande unufaike kupitia ushirikiano huo.

Naye Mwakilishi Mkazi Mwandamizi  wa Shirika  la Kimataifa  la Maendeleo  la Japani nchini (JICA)  Bw. Toshie Nagase  amesema, vijana 12 waliopata nafasi ya mafunzo nchini Japani kupitia Mpango wa ABE initiative  ni kati ya  52 walioomba nafasi  hiyo, hivyo   hawanabudi kuitumia  fursa hiyo  kujifunza kwa bidii  kwa ajili ya manufaa ya nchi.

Mpango wa  ABE initiative  wa miaka  5  ulianzishwa  nchini  Japani mwaka 2013  na  Waziri Mkuu wa Japani Mhe. Shinzo ABE ambaye alitambua umuhimu wa kusaidia uwezeshaji wa maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika, mpango huo ulilenga kunufaisha vijana 1000 wa kiafrika. 

No comments:

Post a Comment