Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo mara baada ya kutia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Sabas (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari iliyofanyika katika ukumbu wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya TEC Bw. Bernard James na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano TEC Bw. Bernard James akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya MawasilianoTEC Bw. Bernard James na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Tumaini Media Padre Joseph Matumaini akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha ujumbe
wa Baba Mtakatifu Papa Fransisko kuhusu maadhimisho ya 5O ya siku ya
Mawasiliano duniani jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Elimu wa Jumuiya za
Kikristo (CSSC) Bw. Petro Pamba akielezea jambo alipokuwa akiwasilisha mada
kuhusu changamoto za mawasiliano katika uinjilishaji mpya wakati wa maadhimisho
ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani leo
Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo jana Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) akichangia mada jana Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) akichangia mada jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Regina Lowassa wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel
akimsikiliza Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Jumbo House of Cameras Bw.
Mathias Luoga(kulia) walipokutana katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari
Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa
Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya TEC Bw. Bernard James,
Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa
Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Saba.
Na Shamimu
Nyaki-WHUSM
KATIBU Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel amewataka
wanahabari nchini kuandika na kuripoti habari
kwa jamii ambazo zina ukweli na zinazotoa elimu kwa jamii kuhusu
maendeleo.
Prof. elisante Ole
Gabriel ameyasema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Upashanaji Habari
Kanisani yaliyofanyika jana Kurasini Jijini
Dar es Salam ambapo amesema wanahabari nchini wanapaswa kutumia vyema taaluma
yao na maadili ya uandishi wa habari.
Aidha Katibu Mkuu
huyo amesema kuwa ni vyema wanahabari kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwa kuitumia
vizuri katika masuala ya kutoa habari
kwa jamii bila kuathiri Utamaduni na amani iliyopo nchini.
“Kuweni makini katika
matumizi ya teknolojia katika kile mnachotaka kuandika ili mlinde Utamaduni
wetu,yale yanayokwenda kwa jamii muyachuje na lazima muyajue vizuri na kwa
usahihi ili kuepuka matokeo hasi kwa jamii”.Alisema Prof.Elisante Ole Gabriel.
Kwa upande wake Padri
Joseph Matuamaini ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media amesema kuwa vyombo
vya habari lazima viwe na Sera na Dira
ambayo inaeleweka kwa watazamaji ili iwe rahisi kuelewa ujumbe wanaoufikisha.
“Vyombo vya habari vya
kidini kuweni na huruma kama Baba wa Mbinguni ,lazima mufikishe ujumbe kwa
jamii kuhusu Utukufu wa Mungu na umuhimu wa amani ili kuondoa hofu kwa
wananchi”.Alisema Padri Matumaini.
Rais alipotangaza
Serikali kuhamia Dodoma wananchi waliingiwa na hofu,lakini hakuna sababu ya
kuogopa bali tuamini kuwa ni hatua nzuri ya kuleta maendeleo na kutimia kwa
ndoto ya muda mrefu ya Taifa letu.
Maadhimisho hayo yalibeba pia ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa
Francis mabao umesisitiza namna bora ya kutumia mawasiliano katika kutangaza mambo mazuri ya Mungu kwa
jamii.

No comments:
Post a Comment