TANGAZO


Thursday, August 4, 2016

WALINZI WAAMUA KUFUNGA OFISI YA WALIMU SHULE YA MSINGI MEDELII DODOMA WAKISHINIKIZA KULIPWA MISHAHARA YAO

Mlinzi wa Shule ya Msingi Medelii iliyopo katika mji wa Dodoma Zebedayo Bendera akifungua mlango wa ofisi ya walimu shuleni hapo mbele ya waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambapo mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Rehema William alifungiwa ndani ya ofisi hiyo ambayo hata hivyo haina usama kutokana na kutokuwa na madirisha. 
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Medelii, Anthonia Komba akisahisha madafutari ya wanafunzi chini ya mti mara baada ya walinzi wa shule hiyo, kuamua kufunga mlango wa Ofisi ya walimu  wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya miezi 7 ambapo kila mwezi hulipwa 70,000. 

Walimu wa Shule ya msingi Medelii iliyopo manispaa ya Dodoma wakifanyia kazi zao chini ya mti kutokana na Mlinzi wa Shule hiyo Kuamua kuwafungia Ofisi yao akishinikizwa kulipwa Fedha zake za mshahara za kipindi cha miezi 7. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment