Sehemu nyingi nchini Kenya zimekumbwa na ukosefu umeme asubuhi ya leo.

Kampuni ya uzalishaji umeme nchini Kenya, imesema ukosefu huo wa umeme umesababishwa na hitilafu za kimitambo katika laini yake kuu.
Wakenya katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakisisitiza kusitisha kuondolewa kwa muhudumu mmoja wa kutoa huduma ya umeme .
Kampuni ya umeme ya Kenya Power, imesema katika taarifa yake kwamba kulikuwa na hitilafu za kimitambo zilizosababisha ukosefu wa umeme mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.
Masaa manne baadaye, kampuni hiyo imesema imerekebisha hitilafu hiyo katika sehemu za magharibi na kati mwa Kenya, lakini katika mji mkuu na maeneo ya mashariki bado wako gizani.
Shida kama hiyo inapotokea wafanyibiashara hutumia mbinu mbadala ya kutumia Jenereta, ingawaje bado hushuhudia hasara kwa kiwango cha juu.

No comments:
Post a Comment