TANGAZO


Saturday, August 20, 2016

SIMBA YAANZA LIGI KUU YA VODACOM, YAITANDIKA NDANDA MABAO 3-1 UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

Mashabiki na wanachama wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo dhidi ya Ndanda FC, uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa Matokeo ukionesha Simba 1 na Ndanda 1. hadi kinamalizika kipindi cha kwanza. Goli la Simba lilifungwa na mchezaji wao mpya, Laudit Mavugo. 
Laudit Mavugo (kulia) akipiga shuti katikati ya wachezaji wa Ndanda FC. 
Jamal Mnyate wa Simba akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Bakari Mtama wa Ndanda FC. 
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akijaribu kumpiga chenga Bakari Mtama wa Ndanda FC.  
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akimpiga chenga Bakari Mtama wa Ndanda FC.  
Mohamed Hussein wa Simba akimtoka Bakari Mtama wa Ndanda FC.
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akijaribu kumpiga chenga Hemedi Khoja wa Ndanda FC. 
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akimpiga chenga Hemedi Khoja wa Ndanda FC.  
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akimtoka Hemedi Khoja wa Ndanda FC.  
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akiwatoka wachezaji wa Ndanda FC. 
Jamal Mnyate wa Simba (kulia), akimtoka Hemedi Khoja wa Ndanda FC.  
Hemedi Khoja wa Ndanda FC, akimkata kwanja Jamal Mnyate wa Simba, wakati akimtoka kuelekea golini kwa timu hiyo. .  
Fredric Blagnon wa Simba akishangilia bao la pili, aliloifungia timu yake akiwa na mwenzake, Laudit Mavugo.
Fredric Blagnon (kulia) wa Simba akishangilia bao la pili na wenzake, aliloifungia timu yake hiyo.
Laudit Mavugo. akimtoka Forahim Isihaka wa Ndanda FC baada ya kumpiga chenga, huku akichanja mbuga kuelekea golini kwa timu hiyo.
Shiza Kichuya wa Simba akishangilia bao la tatu aliloifungia timu yake hiyo katika mchezo huo. 
Shiza Kichuya (kushoto) na Laudit Mavugo wa Simba wakishangilia bao la tatu, aliloifungia timu yake hiyo katika mchezo huo.    
Hadi mwisho, Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 3 na Ndanda FC bao 1.

No comments:

Post a Comment