Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa
Wataalamu wa upimaji Ardhi akiweka alama
katika eneo lililorasimishwa.
Fatma
Salum-Maelezo
|
SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya ardhi na
kuweka huduma za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro ya maji ya mvua
ili kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa
hatimiliki.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela kutoka Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda wakati wa mkutano na
vyombo vya habari.
Akifafanua
Mlonda alisema kuwa mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na Halmashuri zote
za Jiji la Dar es salaam na tayari zoezi limeanza katika Halmashauri ya Manispaa
ya Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono juhudi
hizo za Serikali.
Akizungumzia
vigezo vinavyofuatwa katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela, Mlonda
alibainisha kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa ajili ya
matumizi ya makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master Plan).
“Mpango huu ni shirikishi, wananchi
wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalamu kubainisha mahitaji
ya huduma za jamii na miundombinu na siyo makazi holela yote yana sifa ya
kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.
Aidha,
alisema kuwa eneo husika ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi
katika eneo hilo ambao hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi hata
kama wanalipia ada.
Kigezo
kingine ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo husika
na idadi kubwa ya wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.
“Kuna
maeneo mengi ambayo wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao na
ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa kasi
kubwa; ndio maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa kurasimisha ili
watu wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.
Pia
idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii
wamehamasika na wako tayari kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa
kuchangia gharama za kupanga, kupima na kumilikisha.
Mlonda
alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa
kutatua migogoro ya mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara kwani ndio
msingi wa ufanisi katika zoezi la urasimishaji makazi.
Makazi
holela ni makazi ambayo yamejengwa bila kufuata Sheria, kanuni na taratibu za
Mipangomiji. Ujenzi mijini unaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya
mwaka 2007 na ile ya Serikali za Mitaa sehemu ya mamlaka za miji ya mwaka
1982. ambazo zinaelekeza kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba.
|
|



No comments:
Post a Comment