TANGAZO


Tuesday, August 23, 2016

CHADEMA YAELEZEA MAENDELEO YA MATAYARISHO YA MAANDAMANO YA UKUTA YA SEPTEMBA MOSI, 2016

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Dar es Salaam, Benard Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu maendeleo ya matayarisho ya maandamano ya Ukuta kupinga kile walichokieleza kuzuiwa kufanya siasa hadi 2020, yatakayofanyika Septemba Mosi, 2016 nchini kote. Kushoto ni Katibu wake, Henny Kileo na kulia ni Mjumbe wa chama hicho, Iddi Mauta. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Dar es Salaam, Henny Kileo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano wa kuelezea maendeleo ya matayarisho ya maandamano ya Ukuta yatakayofanyika Septemba Mosi, 2016 nchini kote. Katikati ni Mwenyekiti wake,  Benard Mwakyembe na kulia ni Mjumbe wa chama hicho, Iddi Mauta. 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mkutano huo, wakichukua taarifa hiyo leo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Dar es Salaam, Benard Mwakyembe, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa kichama wa Kinondoni, Mbusule Christopher. 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Dar es Salaam, Henny Kileo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano wa kuelezea maendeleo ya matayarisho ya maandamano ya Ukuta yatakayofanyika Septemba Mosi, 2016 nchini kote. Kulia ni Mwenyekiti wake,  Benard Mwakyembe na kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa kichama wa Kinondoni, Mbusule Christopher. 

No comments:

Post a Comment