Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa taasisi binafsi inayojihusisha na biashara Namaingo Business Agency Bi. Biubwa Ibrahim akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima (NIC) Bw. Sam Kamanga akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es Salaam.
Wadau
mbalimbali wa uchumi nchini wakifuatilia kwa makini majadiliano ya wachngiaji
mada wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania
Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es Salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
SERIKALI imesisitiza matumizi ya bidhaa za ndani ya nchi zinazotengenezwa na watanzania
ili kukuza uchumi wa nchi na kupanua ukubwa wa masoko ili kuleta maendeleo.
Akizungumza
hayo wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa
watanzania Katika uwekezaji Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa
amesema kuwa watanzania wajifunze kupenda na kutumia bidhaa za ndani ili kuweza
kuinua nchi kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa letu.
“Ni lazima
watanzania tujifunze kubadilika kifikra na kimtazamo katika kutumia bidhaa
zilizopo nchini kuchangia Katika kukuza uchumi wa nchi yetu ili kupiga hatua
Katika maendeleo ya Tanzania”alisisitiza Bw.Uledi.
Aidha Bw.
Uledi amesema kuwa mwekezaji yeyote awe wa ndani au wa kigeni anapaswa kutumia
wafanyakazi wa nchini kama kama anataka kuwekeza Katika Taifa letu ili kutoa
fursa kwa watanzania kushiriki Katika kuinua uchumi.
“Mwekezaji
wa kigeni au wa ndani inampasa atumie wataalamu na wafanyakazi wa Tanzania kama
anataka kuwekeza nchini mwetu ili vijana wetu wa kitanzania wapate fursa ya
kuchangia Katika kuinua uchumi wa nchi”.aliongza Bw. Uledi.
Mbali na
hayo Bw. Uledi Mussa amesema kuwa kiwanda chochote kinachowekeza nchini
wanapaswa kutumia malighafi kutoka Tanzania ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo
Katika Taifa letu kwa ujumla.
Naye Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la
uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi.
Beng’i Issa amesema kuwa Katika mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Ongeza Ushiriki Inua Uchumi” umetoka
na mkakati wa kuhakikisha makampuni yote ya uwekezaji kutoka nje yajiandikishe
Katika soko la Hisa (DSE) ili kuongeza ushirikina umiliki wa watanzania Katika
makampuni husika.
Aidha bi.
Issa ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuwa wakandarasi wote ambao wa ndani
wanapewa malipo yao kwa wakati kama walivyokubaliana ili kumsaidia mtanzania
kushiriki Katika kukuza uchumi wa nchi.

No comments:
Post a Comment