Ofisi
ya Waziri Mkuu inapenda kuutaarifu umma kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Prof.
Samwel Mwita Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanzia tarehe tarehe 30 Mei, 2016 kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Uteuzi
huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake katika Sheria ya Msimamizi na
Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Na.5/2012. (The Social Security Laws (Amendements) Act.2012 jedwali la pili
(Second Schedule) kifungu cha 2 (1).
Aidha,
kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb.) amewateua
wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
|
1.
|
Bw. Paul Daud Sangize
|
-
|
Mwakilishi wa Wafanyakazi
|
|
2.
|
Bw. Noel Nchimbi
|
-
|
Mwakilishi wa Wafanyakazi
|
|
3.
|
Bw. David Magese
|
-
|
Mwakilishi wa Waajiri
|
|
4.
|
Bibi Margreth Chacha
|
-
|
Mwakilishi wa Waajiri
|
|
5.
|
Bw. Justine Mwandu
|
-
|
Mwakilishi wa Sekta
Binafsi
|
|
6.
|
Bw. Gabriel Pascal Malata
|
-
|
Mwakilishi wa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
|
|
7.
|
Bw. Emmanuel Maduhu Subi
|
-
|
Mwakilishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango
|
|
8.
|
Bw. Ally Ahmed Msaki
|
-
|
Mwakilishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
|
Imetolewa
na,
Eric F. Shitindi
KATIBU
MKUU
(KAZI,
VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
DAR
ES SALAAM
28/06/2016

No comments:
Post a Comment