Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, akifunga warsha ya Wabunge.
Baadhi ya Wabunge wakiwa katika warsha hiyo.
Na DaudiManongi-Dodoma
Waziri wa Nchi na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi
cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa Halmshauri itakayofanya vizuri.
Waziri Makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa Wabunge kuhusu kukabiliana na tishio
la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge wa
Pius Msekwa mjini Dodoma.
Aidha, amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya Elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hii kuanzia kati kangazi ya chini.
Mhe. Mkamba alisema kuwa upandaji wa miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani
Nyanja
za Afya, ufugaji, misitu, utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.
Aidha, waziri huyo, mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira.
Pia ameahidi Serikali kutenga fedha za kutosha, kutengeneza
Sera nzuri, sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.
Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazohusiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visikihai.
Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa serikali ina mkakati mkubwa wa uboreshaji wa
Sera za Mazingira huku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021, ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya
Tanzania kuwa ya Kijani.
Warsha hiyo, kwa Wabunge imeeandaliwa na Shirika
la Lead Foundation huku ikishirikisha Ofisi ya Bunge na wadau kutoka World Vision,
Ever Green na World Agroforestry Center, ambao walitoa mada mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya kuhifadhi Uoto wa Asili, Kilimo
cha kijani, namna ambavyo ufufuaji wa Visiki hai na Ngitili zinavyoweza kuchangia Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na kuimarisha mshikamano kitaifa wa ustawishaji Miti.

No comments:
Post a Comment