
Serena Williams na Andy Murray wamefanikiwa kutinga katika mzunguko wa pili wa michuano ya Wimbledon inayoendelea mjini London. Kwa upande wa Serena yeye amemchakaza Amra Sadikovic kwa seti 6-2,6-4 huku Murray akimchapa Liam Broady kwa seti 6-2 6-3 6-4 katika mchezo uliokuwa wa kukata na shoka.
Katika mzunguko wa pili Serena Williams atacheza dhidi ya Christina McHale huku Andy Murray mwenye miaka 29 akikipiga na Yen-Hsun Lu kutoka china.


No comments:
Post a Comment