Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, Bungeni Mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (Kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss Nyimbo, mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mjini Dodoma leo.
Waziri wa Fedha na MIpango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, wakiwa makini kuandika hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.
IMAG 7791 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaaban.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (Kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss Nyimbo, mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mjini Dodoma leo.
Waziri wa Fedha na MIpango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, wakiwa makini kuandika hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.
IMAG 7791 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaaban.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma mara baara ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo.
1 JUNI, 2016
1.0 UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika,
kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea,
kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na
Mipango kwa mwaka 2016/17.
2.
Mheshimiwa Spika, naomba
kuanza hotuba yangu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuniruhusu kusimama
mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa
mwaka 2016/17.
3.
Mheshimiwa Spika, napenda kutumia
fursa hii adhimu kuwapongeza kwa dhati kabisa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Samia Suluhu Hassan,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi mkubwa waliopata
katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuwawezesha kuongoza Taifa
letu na Serikali ya Awamu ya Tano. Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Mhe. Kassim
M. Majaliwa kwa kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kura nyingi kuwa
Mbunge wao na hivyo kutoa fursa kwa yeye kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa pamoja, nawaombea afya njema
na hekima kutoka kwa Mungu katika kutekeleza majukumu yao chini ya kaulimbiu ya
“Hapa Kazi Tu” kwa manufaa ya
wananchi wote na hasa masikini.
4.
Mheshimiwa Spika, naomba nikupongeze
wewe binafsi kwa kuchaguliwa kwako kuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kuliongoza Bunge letu
Tukufu kwa busara na hekima. Aidha, nampongeza pia Mhe. Dkt. Tulia Ackson
Mwansasu, kwa kuteuliwa kuwa mbunge na kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika na
hivyo kukusaidia kuendesha vyema shughuli za Bunge. Nawaombea kwa Mungu awape
afya na hekima ya kuendesha Bunge hili kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
5.
Mheshimiwa Spika,
naomba kuchukua fursa hii pia kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa
kuchaguliwa kuwakilisha wananchi wa majimbo yenu na wote walioteuliwa
kuwakilisha makundi maalum katika jamii yetu. Aidha, nawapongeza Mawaziri na
Naibu Mawaziri wote wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuaminiwa na kuteuliwa na
Mheshimiwa Rais kumsaidia katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
6.
Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoe
shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Fedha
na Mipango. Hivyo, kwa mara nyingine, ninamuahidi Mheshimiwa Rais na Watanzania
kwa ujumla kwamba nitatekeleza jukumu hili kwa bidii, weledi na uadilifu.
7.
Mheshimiwa Spika, kipekee
nimshukuru Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba
Kijaji – Mbunge wa Kondoa, kwa ushirikiano anaonipa kutekeleza majukumu yangu
kwa ufanisi mkubwa. Aidha, niwashukuru
pia Viongozi wa Wizara, nikianza na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali,
Dkt. Servacius Beda Likwelile, Naibu Makatibu Wakuu, Ndugu Dorothy S. Mwanyika,
Ndugu James Doto na Ndugu Amina Kh. Shaaban, kwa ari yao ya kujituma katika
kutekeleza majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango. Vilevile napenda kuwashukuru Prof. Benno
Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Lawrence Mafuru - Msajili wa Hazina na Dkt.
Albina Chuwa - Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa kunisaidia
kutekeleza majukumu yangu vizuri na kuongoza taasisi muhimu wanazosimamia kwa
weledi mkubwa. Aidha, nawashukuru Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi,
Wakuu wa Vitengo na Wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kazi
nzuri na ushirikiano wao mkubwa wanaonipatia katika kutekeleza majukumu yetu ya
kila siku.
8.
Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru
kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa
Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini, na Makamu Mwenyekiti
Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo kwa ushirikiano wao
waliotupatia wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara
yangu. Ninaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana na Kamati hii na kuzingatia
ushauri na maelekezo wanayotupatia kwa lengo la kuleta ufanisi katika
kutekeleza majukumu ya Wizara yangu.
9.
Mheshimiwa Spika,
hotuba yangu itajikita katika maeneo makuu matatu yafuatayo: Kwanza, ni
Mwelekeo wa Majukumu ya Wizara katika Kujenga Msingi wa Uchumi Imara. Pili, Mapitio
ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2015/16 na tatu, Malengo na Maombi
ya Fedha kwa mwaka 2016/17.
2.0 MWELEKEO KATIKA KUJENGA MSINGI WA UCHUMI IMARA
10.
Mheshimiwa Spika, azma
ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia azma hii, ni muhimu kuwekeza katika
viwanda kama ilivyosisitizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli wakati akizindua Bunge la 11 tarehe 20 Novemba,
2015.
11.
Mheshimiwa Spika,
wakati Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa
(Mb), alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Bunge lako Tukufu mnamo tarehe
25 Aprili 2016, alielezea mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano yenye falsafa
ya HAPA KAZI TU nanukuu “Malengo ya
Serikali ya Kufikia kipato cha kati na kufanyika mapinduzi makubwa ya viwanda
yanategemea sana utulivu wa uchumi”, mwisho wa kunukuu.
12.
Mheshimiwa Spika,
Wizara yangu imejipanga kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kujenga Taifa
linalojitegemea kwa kukuza uchumi na kupunguza umasikini. Moja ya hatua hizo ni kusimamia na kufuatilia
kwa ukamilifu utekekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano
2016/17 - 2020/21. Mpango huu unajikita katika kujenga msingi wa uchumi wa
viwanda na maendeleo ya watu.
13.
Mheshimiwa
Spika, ili mpango huu uweze kutekelezwa kwa ufanisi na kupata
matokeo tarajiwa, ni dhahiri kuwa tutahitaji rasilimali za kutosha, hususan
rasilimali fedha. Wizara ya Fedha na
Mipango kwa kushirikiana na wadau wengine inalo jukumu la kuimarisha ukusanyaji
wa mapato ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimali fedha. Aidha,
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 imeweka bayana
majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango ya kuimarisha usimamizi na ukusanyaji wa
mapato, kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na kusimamia kwa ufanisi
matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali.
14.
Mheshimiwa Spika, kwa
upande wa kuimarisha usimamizi na ukusanyaji wa mapato, Wizara itajielekeza
katika maeneo yafuatayo:- Kusimamia
kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa
mapato ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato; Kurasimisha sekta
isiyo rasmi kuingia katika mfumo wa kodi na hivyo kupanua wigo wa kodi na; Kuimarisha
ufuatiliaji wa mapato yanayokusanywa na taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali
ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Tunalenga pia kuimarisha
ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na kuboresha usimamizi wake chini ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania kutokana na uzoefu na mifumo ya ukusanyaji iliyopo
nchi nzima; Kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi
isiyo na tija; na Kuendelea kuimarisha usimamizi na kufanya ukaguzi wa mara kwa
mara bandarini na maeneo ya mipakani ili kuhakikisha kwamba kodi stahiki
zinakusanywa.
15.
Mheshimiwa Spika, mikakati
mingine itakayotekelezwa na Wizara ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha
hotuba yangu kuanzia ukurasa wa saba hadi
ukurasa wa kumi.
16. Mheshimiwa
Spika, sambamba
na mikakati niliyoitaja hapo juu, majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango yatakayotekelezwa
ili kufikia azma ya kujenga msingi wa uchumi imara na Taifa linalojitegemea ni
kama pia inavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 11.
3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2015/16
17. Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2015/16, majukumu ya Wizara yaliendelea kutekelezwa kupitia
mafungu tisa ya kibajeti na taasisi na mashirika 35 yaliyo chini yake (Jedwali
na.1). Mafungu hayo ni Fungu 50 - Wizara ya Fedha na Mipango; Fungu 21 –
Hazina; Fungu 22 - Deni la Taifa; Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali;
Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha; Fungu 13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; Fungu 7 – Ofisi ya
Msajili wa Hazina; Fungu 66 – Tume ya Mipango na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi.
18.
Mheshimiwa Spika, ili
kufikia lengo kuu la kusimamia utekelezaji wa sera za uchumi jumla, mipango ya Wizara
katika mwaka 2015/16, mapato ya Wizara kwa mwaka 2015/16 pamoja na matumizi ni
kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 12 hadi
ukurasa wa 16.
3.1 UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2015/16:
19.
Mheshimiwa Spika, napenda
sasa kuchukua fursa hii kuelezea kwa kina utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa
mwaka 2015/16.
3.1.1 Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla
20. Mheshimiwa
Spika, Wizara imesimamia utekelezaji wa Sera na Mikakati ya uchumi
jumla zikiwemo Sera za Kibajeti na zile za Kifedha (Fiscal and Monetary
policies) ili kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaendelea kukua na hivyo kunufaisha
wananchi walio wengi zaidi. Sera ya
bajeti inalenga, pamoja na mambo mengine, kudhibiti na kupunguza mfumuko wa bei
na hivyo kupunguza gharama za maisha ya wananchi.
3.1.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa
21. Mheshimiwa Spika,
Wizara imeendelea kuratibu uandaaji na ufuatiliaji wa mipango ya maendeleo
nchini sambamba na kusimamia uchumi. Ili kutekeleza majukumu hayo, Wizara
imekamilisha uandaaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 –
2020/21) na tayari umeidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Aidha, Wizara imeandaa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17. Mpango huu ni wa kwanza katika
kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Mwaka 2016/17 – 2020/21.
22. Mheshimiwa
Spika, mikakati maalum iliyozingatiwa katika Mpango wa Mwaka 2016/17 pamoja
na shughuli nyingine zilizotekelezwa ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha
hotuba yangu ukurasa wa 17 na
ukurasa wa 18.
3.1.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini
23. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2015/16, Wizara iliendelea
kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa MKUKUTA-II ikiwa ni pamoja na kufanya
tathmini ya mkakati huo ambao baada ya kuongezewa muda wa mwaka mmoja wa
utekelezaji, unafikia ukomo wake mwezi Juni, 2016. Matokeo ya tathmini hiyo
yameainishwa katika Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA-II kwa kipindi cha Miaka
Mitano (2010-2015). Taarifa hii ilisambazwa kwa Waheshimiwa Wabunge wakati
nilipowasilisha mwelekeo wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya Pili
(2016/17 - 2020/21) kwenye semina ya Waheshimiwa Wabunge mwezi Februari, 2016.
Tathmini hiyo imetoa mchango mkubwa katika kubainisha vipaumbele vya Mpango wa
Maendeleo Awamu ya Pili ambao umejumuisha masuala ya kupambana na umaskini.
24. Mheshimiwa Spika, kwa ufupi, mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji
wa MKUKUTA-II ni pamoja na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania kutoka shilingi
770,464.3 mwaka 2010 kufikia shilingi 1,918,928 mwaka 2015; kuongezeka kwa kasi
ya kupungua kwa umaskini wa kipato ambapo kati ya mwaka 2007 na 2012 umasikini
ulipungua kwa asilimia 6.2, kutoka asilimia 34.4 hadi asilimia 28.2,
ikilinganishwa na kupungua kwa kiwango cha asilimia 4.6 katika kipindi cha
miaka 15, yaani kutoka asilimia 39 mwaka 1992 hadi kufikia 34.4 mwaka 2007.
25. Mheshimiwa Spika, umri wa mtanzania wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 51
mwaka 2001 hadi miaka 61 hivi sasa. Mafanikio hayo kwa pamoja yamechangia
kupandisha Kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (Human Development Index - HDI)
kutoka asilimia 48.8 mwaka 2014 hadi asilimia 52 mwaka 2015.
3.4.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali
(a) Mapato ya Ndani
26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Sera za Mapato zililenga kukusanya
mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi
bilioni 13,999.52 (ikijumuisha mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa).
Hadi kufikia Machi, 2016 jumla ya makusanyo ya ndani (ikijumuisha mapato ya Mamlaka ya Serikali za
Mitaa) yalikuwa shilingi bilioni
10,346.55 sawa na asilimia 74 ya
makadirio ya mwaka.
27. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya kodi, Wizara imeingia
mikataba ya kiutendaji na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanzia ngazi ya juu mpaka
wasimamizi wa chini; kupitia TRA, Wizara imeendelea kuimarisha matumizi ya
mashine za kielektroniki (EFD) ikiwa ni pamoja na kuanza kutoa mashine hizo
bure kwa wafanyabiashara na kupiga marufuku Taasisi, Wakala wa Serikali, na Mamlaka
za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni ambao hawatumii mashine hizo;
kuboresha matumizi ya mfumo wa TANCIS pamoja na Mfumo Mmoja wa Ukadiriaji wa
Thamani za Bidhaa; Kuwatambua walipa kodi kupitia tafiti mbalimbali na hatimaye
kuwasajili; na Kutekeleza utaratibu wa ulipaji kodi kwa kutumia vitalu vya kodi.
28. Mheshimiwa Spika, hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na: kuwatambua
na kuwasajili wajasiriamali walio kwenye sekta isiyo rasmi na kufuatilia
mwenendo wa malipo yao; Kutekeleza mkakati wa ulipaji kodi kwa hiari; Kufanya
utafiti kuhusu kodi za pango za majengo ambazo zinatoa mwelekeo wa kodi za
mapato kutoka kwa wenye majengo ya biashara; Kutumia mifumo ya TEHAMA katika
kusajili na malipo ya kodi; na uwasilishaji kwa njia ya kielektroniki wa Ritani
za kodi ya ongezeko la thamani na
miamala ya forodha. Aidha, Serikali ilikamilisha Sheria ya Usimamizi wa Mapato
ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015 yenye lengo la kuhakikisha kuwa matumizi ya
mapato yatokanayo na mafuta na gesi yatasimamiwa ipasavyo kwa manufaa ya kizazi
cha sasa na vizazi vijavyo.
29. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi Wizara
imesimamia na kuhimiza utumiaji wa mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa
risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali Kuu, Mamlaka za
Serikali za Mitaa na Mawakala wote wa Serikali. Aidha, Wizara imeendelea
kuhimiza uongezaji wa kufanya uthamini wa majengo mijini ili kuhakikisha
ulipaji wa viwango stahiki; na kusimamia kwa karibu zaidi Mashirika ya Umma na
Wakala wa Serikali ili kuhakikisha Serikali inapata gawio stahiki, matumizi
yasiyo na tija yanaondolewa na mapato ya ziada yanachangia Mfuko Mkuu wa
Serikali.
(b) Misaada na Mikopo
30. Mheshimiwa Spika, Wizara ililenga kuendeleza ushirikiano na wadau
mbalimbali wakiwemo Washirika wa Maendeleo katika kutekeleza mipango ya
maendeleo. Katika mwaka 2015/16, Washirika wa Maendeleo waliahidi kuchangia
bajeti ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
bilioni 2,322.5 ambapo misaada ya Kibajeti ni shilingi bilioni 660, Mifuko ya kisekta ni shilingi bilioni 199 na miradi ya Maendeleo ni shilingi bilioni 1,463.
31. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2016 kiasi cha shilingi bilioni 1,064.89 sawa na asilimia 46 kimepokelewa. Kati ya kiasi hicho, Misaada ya kibajeti
ni shilingi bilioni 169.6 (sawa na
asilimia 26 ya ahadi), Mifuko ya kisekta ni shilingi bilioni 243.96 (sawa na asilimia 123 ya ahadi) na Miradi
ya Maendeleo shilingi bilioni 651.32
(sawa na asilimia 46 ya ahadi).
32. Mheshimiwa Spika, kupungua kwa misaada toka nje kunatokana na kujiondoa
kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo wanaochangia kupitia Misaada na mikopo ya
kibajeti na baadhi ya Washirika wa Maendeleo kupunguza ahadi zao. Wafadhili
wanaochangia kupitia misaada ya kibajeti walipunguza michango yao kutoka shilingi bilioni 660 mpaka shilingi bilioni 399 katikati ya mwaka
wa fedha 2015/16 na wengine kuhusisha utoaji wa fedha na masharti ambayo hayakuwemo
katika makubaliano ya awali. Katika kushughulikia changamoto hizi, Serikali
inaendelea na mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ili kuhakikisha kwamba fedha
zilizoahidiwa zinatolewa kwa wakati.
3.4.5.1.
Uandaaji
na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya
Serikali
33. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu la Uandaaji na Usimamizi wa
Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, Wizara imeratibu uandaaji wa Mwongozo wa
Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/17 pamoja na Kitabu cha Taarifa ya Hali ya Uchumi
kwa mwaka 2015 na; kufanya marekebisho ya takwimu za Bajeti ya Mafungu
mbalimbali kwenye mfumo wa IFMS na kuchapisha vitabu vya bajeti ya mwaka wa
fedha 2015/16 (Juzuu Na. II, III & IV). Aidha, Wizara iliandaa, kuchapisha
na kusambaza kitabu cha tafsiri rahisi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha
2015/16 yaani “Citizen’s Budget”; na kuendesha mafunzo ya wakufunzi wa kitaifa wa
Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 na kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kwa Mikoa
26, Halmashauri 182, pamoja na Wizara zote nchini.
34. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha usimamizi wa bajeti hasa kwenye miradi
ya maendeleo unazingatiwa, Wizara ilifanya ufuatiliaji wa fedha za Mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu; mapato na matumizi ya VETA; fedha za ‘Skills Development
Levy’ kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania. Aidha, Wizara ilihakiki madeni ya Shirika
la Habari Tanzania (TBC), Kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN), Kampuni ya Simu
(TTCL) yanayodaiwa katika Taasisi mbalimbali za Serikali na Shirika la
kudhibiti nzige wa jangwani na nzige wekundu. Wizara pia ilifanya ufuatiliaji
wa fedha za SDL zilizotolewa kwenye mradi wa “Support Skills Development
Project” kwa Wizara ya Kazi.
3.4.6. Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma
35. Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti matumizi ya fedha za umma, Wizara
kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali imeendelea kufanya ukaguzi
maalum katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Jukumu hilo limetekelezwa kwa kufanya uhakiki wa
madai ya walimu na watumishi wasio walimu wa Serikali, watoa huduma ya chakula
katika shule za msingi na sekondari za Serikali, madai ya Wakandarasi, Washauri,
madai ya fidia, mirahaba na gharama za usimamizi wakati wa utekelezaji wa
miradi ya barabara.
36. Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizofanywa chini ya Usimamizi na
Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha
hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 26 hadi na 28.
3.4.7. Usimamizi wa Malipo
37. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwa
watumishi 238 wa kada ya uhasibu, ugavi, uchumi na kompyuta kutoka kwenye Wizara, Idara za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Manispaa,
Halmashauri za miji; na Watumishi wapatao 650 wa kada ya uhasibu wamepatiwa
mafunzo ya kutayarisha hesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa vya Uhasibu
(IPSAS Accrual). Aidha, Mfuko wa Bunge umeunganishwa kwenye Mtandao wa Malipo
wa kielektroniki wa TISS pamoja na EFT; Malipo ya Mirathi (Death Gratuity)
yameunganishwa kwenye mfumo wa “Electronic Fund Transfer”. Mfumo huu umewezesha
malipo kuingizwa kwenye akaunti za benki za warithi moja kwa moja na hivyo
kuharakisha malipo. Wizara imeendelea kusimamia uendeshaji mtandao wa malipo wa Serikali (Integrated
Financial Management System – IFMS) kwa
kutoa ushauri wa kitaalamu na kuziwezesha Idara/Wizara za Serikali
pamoja na Mikoa kutumia mtandao kwa
ufanisi. Pia kutatua matatizo ya kiufundi pale yanapotokea.
3.4.8.
Deni la Taifa
38. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kusimamia Deni la Taifa kwa
kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada SURA 134. Aidha, msisitizo
umewekwa kukopa mikopo yenye masharti nafuu ambayo inakopwa kwa uangalifu na
kutumika kwenye miradi yenye vichocheo vya ukuaji wa uchumi, ikiwemo ujenzi wa
miundombinu ya barabara, reli, ujenzi wa mitambo ya kufua umeme na ujenzi wa
viwanja vya ndege.
39. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2015/16, Serikali ilitenga shilingi bilioni
504.57 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la nje. Hadi Machi, 2016 shilingi
bilioni 414.66 sawa na asilimia 82 zilitumika kwa ajili hiyo. Aidha, Serikali
ilitenga shilingi bilioni 899.89 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani.
Hadi Machi, 2016 shilingi bilioni 547.88 sawa na asilimia 61 zilitumika kwa
ajili hiyo.
40. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2015/16 Serikali ilitenga pia shilingi
bilioni 421.20 kwa ajili ya kulipa mtaji wa deni la nje. Hadi Machi, 2016
shilingi bilioni 395.90 sawa na asilimia 94 zilitumika kwa ajili hiyo. Aidha,
Serikali ilitenga shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya kulipa mtaji wa deni la
ndani. Hadi Machi, 2016 shilingi trilioni 1.86 sawa na asilimia 69 zilitumika
kwa ajili hiyo.
3.4.9. Usimamizi wa Mali ya Serikali
41. Mheshimiwa Spika, katika jukumu la usimamizi wa mali ya Serikali, Wizara
imefanya uthamini wa ardhi, majengo na mali nyingine za Serikali ambapo taasisi
kumi zinaendelea kufanyiwa uthamini; Kuondosha mali chakavu katika Wizara na Idara
za Serikali ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.06 zilikusanywa kutokana na
mauzo ya magari na vifaa chakavu; na vibali vya uondoshaji wa mali chakavu
vilivyokuwa na thamani ya shilingi bilioni 1.68 vilitolewa kwa mamlaka na
taasisi mbalimbali za Serikali.
3.4.10. Ununuzi wa Umma
42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Wizara imepitia Sheria ya Ununuzi
wa Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 na kupendekeza marekebisho ya sheria hiyo; Kukamilisha
uandaaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma na mkakati wa utekelezaji wake; Kuanza
kutekeleza mpango wa mahitaji ya mafunzo wa maafisa ununuzi na ugavi kwa
kuwajengea uwezo wa namna ya kupunguza vihatarishi katika ununuzi wa umma; Kuhakiki
taarifa za maafisa ununuzi na ugavi na
kuziweka katika daftari la maafisa ununuzi na ugavi Serikalini pamoja na
kukamilisha maandalizi ya kufanya tathmini ya ufanisi wa mfumo wa ununuzi wa umma
nchini.
43.
Mheshimiwa
Spika, shughuli nyingine
zilizotekelezwa chini ya Usimamizi
wa Ununuzi wa Umma, Rufaa za Zabuni za Umma, Huduma ya Ununuzi Serikalini, na
kupitia Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi ni kama inavyooneshwa katika
kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 31 hadi ukurasa wa 36.
3.4.11. Ukaguzi wa Hesabu za Serikali
44. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
ilifanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka
2014/15 kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Aidha, Ofisi ilifanya ukaguzi wa hesabu za Wizara na Idara za
Serikali zinazojitegemea 63, mikoa 25 ya Tanzania Bara; Wakala za Serikali 32,
Mifuko maalum na Taasisi nyingine za Serikali 45, Balozi 34 za Tanzania nje ya
nchi, na hivyo kufanya jumla ya Taasisi zote zilizokaguliwa chini ya Serikali
Kuu kufikia 199. Ukaguzi mwingine ulifanyika kwenye Mamlaka za Serikali za
Mitaa 164 na Mashirika ya Umma 102 kati ya Mashirika 186.
45. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali zilizofanyika
ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 37 hadi
ukurasa wa 39.
3.4.12. Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma
46. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la
kusimamia rasilimali za Serikali ambapo rasilimali hizi ni pamoja na uwekezaji
wa Serikali katika hisa za Mashirika ya Umma na ya Binafsi. Aidha, katika
kutekeleza jukumu hili, Wizara husimamia utendaji wa Mashirika na Taasisi za
Umma na kutoa ushauri kwa Serikali juu
ya uwekezaji wake na nini kifanyike ili
kuimarisha uendeshaji wa Taasisi na
Mashirika ya Umma yanayosimamiwa na Wizara yapatayo 216.
47. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu hili, Wizara kwa mwaka 2015/16
imekamilisha Taarifa ya uwekezaji wa Serikali kwenye Mashirika na Taasisi za
Umma na kuiwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG;
Kukirejesha kwenye umiliki wa Serikali Kiwanda cha General Tyre kwa kununua hisa za mbia; Kukamilisha uhakiki wa madai
wa waliokuwa watumishi kwenye mashirika yaliyobinafsishwa; Kufanya Ukaguzi wa Kimenejimenti
kwenye Taasisi tano ambazo ni Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Kivukoni, Shirika la Elimu - Kibaha, Bodi
ya Kahawa Tanzania na Chuo cha Ubaharia - Dar Es Salaam na Makumbusho ya
Taifa ambapo taarifa ya kaguzi hizo zimeandaliwa.
48.
Mheshimiwa Spika, mambo
makubwa yaliyobainika katika kaguzi hizo za kimenejimenti ni pamoja na:
Matumizi yasiyoridhisha ya rasilimali watu na fedha; ajira zisizozingatia
utaratibu; ulipaji marupurupu na posho usiozingatia utaratibu
na nyaraka za Msajili wa Hazina; madeni
ya wazabuni ya muda mrefu yaliyolimbikizwa kutokana na ukosefu wa fedha,
kutokana na ukosefu wa fedha; baadhi ya Taasisi kuingia mikataba ya
kibiashara ambayo haina maoni ya Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, uendeshaji wa Taasisi bila kuzingatia vigezo
vya utawala bora kwa baadhi ya taasisi na hivyo kushindwa kutumia rasilimali
zilizopo kwa weledi na tija; na Mamlaka za uteuzi kushindwa kuteua Bodi za
Wakurugenzi kwa wakati kwa baadhi ya taasisi na kusababisha maamuzi ya msingi kuchelewa
kufanyika au kutokufanyika kabisa.
49.
Mheshimiwa
Spika, hatua mbalimbali
zimechukuliwa ili kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa katika kaguzi hizo
ikiwemo; kuzijulisha Wizara Mama pamoja na mamlaka nyingine za Serikali matokeo
ya kaguzi hizo ili ziweze kuchukua hatua stahiki kwa Taasisi na Mashirika
wanayoyasimamia; Ofisi ya Msajili wa Hazina kutoa maelekezo ya kusitisha malipo
ya posho yasiyozingatia nyaraka na kanuni za Utumishi na kanuni za fedha,
kuziagiza Taasisi husika kuandaa miongozo inayohitajika katika uendeshaji wa
Taasisi na Mashirika, kuziagiza Bodi za Taasisi kuchukua hatua stahiki dhidi ya
mapungufu yaliyobainishwa kwenye kaguzi na kumuomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kupitia upya mikataba ya kibiashara iliyoingiwa na Taasisi na Mashirika ya
Umma.
50. Mheshimiwa Spika, Wizara pia
ilifanya uperembaji (Monitoring and
Evaluation) kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma 55 yaliyobinafsishwa kwa lengo
la kukagua ufanisi na kuhakiki utekelezaji wa masharti kulingana na mikataba ya ununuzi kwa mujibu wa agizo la
Mheshimiwa Rais wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11. Baadhi ya mashirika hayo ni
Mwanza Textile, Shinyanga Meat, Ilemela Fisheries, Manawa Ginneries, Blanket
Manufacturing, Mtwara Cashewnut Factory, Likombe Cashewnut, Newala I Cashewnut
Factory, Newala II Cashewnut Factory, Mtama Cashewnut Factory, Mufindi Pyrethrum Factory, TTA Dabaga,
Mufindi Tea Company, Ludodolelo Pyrethrum Factory na Mahenye Farm.
Kilichobainika ni kuwa baadhi ya wawekezaji kushindwa kutekeleza masharti ya
mikataba hususan kuwekeza kwa kuzingatia mpango wa uwekezaji uliokubalika kati
ya Serikali na Wawekezaji.
51.
Mheshimiwa
Spika, baada ya uperembaji huu Wizara imechukua hatua
mbalimbali zikiwemo: Kuwaita wawekezaji wote waliobainika kutotekeleza mikataba
ya mauzo; Kutoa notisi ya kusudio la kuvunja mikataba ya mauzo kwa baadhi ya
wawekezaji; Kuvunja mkataba wa mauzo na wawekezaji; Kusaidia kutatua baadhi ya
changamoto ambazo zimesababisha kutotekelezwa ipasavyo kwa mikataba ya mauzo
ikiwemo kutokuwepo mipango wa Uwekezaji; na kuwapongeza baadhi ya wawekezaji ambao
wameendelea kufanya vizuri katika kuendeleza mali walizonunua na kuchochea
shughuli za kiuchumi na hatimaye kuchangia kwenye pato la Taifa.
3.4.13. Mafao ya Wastaafu na Mirathi
52. Mheshimiwa Spika, dhana ya msingi ya sekta ya hifadhi ya jamii imejikita
katika kuhakikisha kuwa wananchi wanawezeshwa kuishi maisha yenye staha kwa kupata
huduma za msingi katika vipindi vya uzee, maradhi, ukosefu wa kazi, uzazi, kifo
na hali nyingine itakayosababisha mtu asiweze kufanya shughuli za kujiongezea
kipato. Serikali kwa kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wastaafu katika
ujenzi wa Taifa imeendelea kuboresha huduma ya malipo kwa wastaafu, kwa kulipa pensheni moja kwa moja kwenye akaunti zao kwa kutumia
mfumo wa TEHAMA wa Benki Kuu ya Tanzania uitwao TACH kuanzia mwezi Mei, 2015.
Aidha kumbukumbu za wastaafu zimeendelea kuhifadhiwa kwenye mfumo wa TEHAMA
unaoitwa SAPERION ambapo hadi Machi, 2016 kumbukumbu za wastaafu 66,666
zilikuwa zimewekwa kwenye mfumo huo.
53. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu huo wa hifadhi ya jamii kwa watumishi
wa Umma na kwa kuzingatia sheria na kanuni za mifuko ya hifadhi ya jamii, Wizara
hadi Machi, 2016 iliwasilisha mchango wa mwajiri kiasi cha shilingi bilioni
274.0.
3.4.14. Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi
54. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2015/16 Wizara kupitia Kitengo cha
Kudhibiti Utakasishaji wa Fedha Haramu imeendelea kusimamia utekelezaji wa
Sheria ya Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu. Hadi kufikia Machi, 2016
Wizara imepokea na kuchambua taarifa 164 za miamala shuku inayohusu fedha
haramu na ufadhili wa ugaidi. Kati ya hizo, taarifa 52 za kiintelijensia
ziliwasilishwa kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa uchunguzi. Aidha, Wizara ilikagua
watoa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na benki 17 na kampuni ya masoko ya hisa
moja.
55. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilisaini Hati za Makubaliano (Memorandam of
Understanding) na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa na Kitengo cha Kudhibiti Utakasishaji wa Fedha Haramu cha
Zimbabwe na hivyo kufanya idadi ya hati za makubaliano na vitengo mbalimbali
kuwa kumi; Kutoa elimu na mafunzo kwa wadau mbalimbali wakiwemo watoa taarifa
za jinsi ya kutumia mfumo maalum wa
uchambuzi wa taarifa wa kompyuta kwa ajili ya kurahisisha uwasilishaji wa taarifa za miamala shuku na uchambuzi; na
Kuratibu na kusimamia zoezi la Kitaifa la kutathmini viashiria hatarishi vya
fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.
3.4.15. Tume ya Pamoja ya Fedha
56.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2015/16 Wizara
kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilisha Ripoti ya Stadi kuhusu Mwenendo wa
Uchumi na Mapato ya Muungano ambayo lengo lake ni kuiwezesha Tume kushauri na
kupendekeza namna bora ya kuboresha vyanzo vya mapato ya muungano kwa
kuzingatia mwenendo wa uchumi. Ripoti ya stadi hiyo imewasilishwa katika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
3.4.16. Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi
57. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imeendelea kupokea na
kuchambua miradi ya ubia kwa lengo la kuiidhinisha kwa mujibu wa Sheria. Wizara
kupitia Kitengo chake cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
imechambua na kuidhinisha mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi lll. Aidha,
upembuzi yakinifu wa mradi wa barabara ya tozo kati ya Dar es Salaam na
Chalinze unaendelea kufanyika. Kadhalika, Serikali ipo katika hatua ya mwisho
kumpata mshauri elekezi kwa ajili ya mradi wa kuzalisha madawa muhimu na utengenezaji
wa vifaa tiba chini ya Bohari Kuu ya Madawa (MSD). Vilevile, Wizara kupitia
kitengo chake cha ubia inafanya uchambuzi wa maandiko ya mradi wa uendeshaji wa
daraja la Kigamboni kwa lengo la kuidhinisha Mradi huo tayari kwa kuandaliwa mkataba
wa uendeshaji.
58. Mheshimiwa Spika, sambamba na uchambuzi wa miradi, katika mwaka 2015/16
mafunzo mbalimbali yalitolewa kwa makundi sita yakiwemo watunga sera; Maofisa Waandamizi Serikali Kuu na Serikali za
Mitaa; Taasisi Binafsi; Mashirika ya Umma; Taasisi za Serikali; na taasisi za
fedha kutegemea na mahitaji na majukumu ya kila kundi. Jumla ya wadau 217 walipatiwa mafunzo kuhusu
Sera, Sheria na Kanuni za Miradi ya Ubia.
3.5. USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA CHINI YA WIZARA
59. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, Wizara yangu inaratibu na
kusimamia mashirika na Taasisi za Umma 35 zilizo chini yake. Utekelezaji wa
majukumu ya Taasisi na Mashirika haya kwa mwaka 2015/16 ni kama inavyooneshwa
katika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 46 hadi ukurasa wa 75. Aidha, utekelezaji wa miradi ya maendeleo
chini ya Wizara kwa mwaka 2015/16, ikijumuisha mafanikio pamoja na changamoto
ni kama pia unavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 76 hadi ukurasa wa 82.
4.0 MALENGO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2016/17
60.
Mheshimiwa Spika, baada
ya kuelezea utekelezaji wa mjukumu ya Wizara kwa kina kwa mwaka 2015/16, naomba
sasa nieleze malengo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2016/17.
4.1 MAJUKUMU YA WIZARA
4.1.1 Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla
61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara imepanga kuendelea
kuimarisha Sera ya fedha ili iendane na sera ya bajeti kwa lengo la kudhibiti
na kupunguza mfumuko wa bei pamoja na tofauti kati ya riba za amana na zile za
mikopo.
4.1.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa
62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara imepanga kuendelea
kuwaelimisha wadau mbalimbali kuhusu wajibu wao katika kutekeleza Mpango wa
Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2020/21); Kuandaa Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017/18;
Kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na; Kuchapisha,
kusambambaza na kuelimisha wadau mbalimbali kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa
Uwekezaji wa Umma (PIM – OM). Shughuli hii inalenga kuimarisha taratibu za uibuaji,
utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa miradi
inayoibuliwa inatekelezwa kikamilifu na kwa mafanikio makubwa.
4.1.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini
63. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa mwaka 2016/17 imepanga kuandaa mpango wa
kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini wa jitihada za kuondoa umaskini, ikiwemo
viashiria vya kupima utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mpango huu
utasaidia kufuatilia utekelezaji wa programu za kuondoa umaskini katika sekta
mbalimbali, kuibua changamoto na kurekebisha kasoro kila mwaka; Kuandaa Taarifa
ya Hali ya Umaskini na Maendeleo ya Watu; Kuanzisha kituo cha utunzaji na
utoaji wa taarifa mbalimbali kuhusu programu za kuondoa umaskini na maendeleo
ya watu; Kuandaa mwongozo wa namna ya kuibua na kutumia fursa za kiuchumi
katika maeneo yanayowazunguka wananchi katika halmashauri mbalimbali nchini.
Hatua hii itaongeza ushiriki wa wananchi hususani vijijini katika miradi ya
uzalishaji na kuongeza kipato; na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya
kuondoa umaskini hususan namna bora na endelevu ya kuboresha jitihada za
Serikali katika kuinua hali ya maisha ya watanzania walio chini ya mstari wa
umaskini na kuongeza kasi katika kuleta maendeleo ya binadamu.
4.1.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali
(a) Mapato ya Ndani
64. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato, katika mwaka
2016/17 Wizara pamoja na mambo mengine imepanga kuendelea na mfumo wa dirisha
moja la kielektroniki kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Mapato;
kuendelea kudhibiti mizigo yote inayoingia kutoka bandari kavu zote; kuendelea
kuimarisha mapato kwenye ushuru wa forodha na bidhaa; kuendelea kusimamia
matumizi ya mashine za kielektoniki (EFDs); kushughulikia kwa haraka rufaa za
pingamizi na kodi; kufanya kaguzi kwa kuzingatia viashiria hatarishi vya
uvujaji wa mapato ya Serikali; kusimamia misamaha ya kodi ili kuhakikisha
inatolewa tu kwa wale wanaostahili na inatumika ipasavyo na; kuendelea kutoa
elimu ya walipa kodi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.
(b) Misaada na Mikopo
65. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Serikali itaendelea kushirikiana na
wadau mbalimbali ili kupata fedha za nje za kugharamia miradi ya maendeleo. Serikali
itaelekeza fedha za nje katika kutelekeza miradi mikubwa ya maendeleo itakayochochea
ukuaji wa uchumi sambamba na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani
na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya Serikali. Hata hivyo, azma ya Serikali
ni kupunguza na hatimaye kuondokana na utegemezi wa kibajeti.
66. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo
tumekubaliana kuwaleta Washauri Elekezi wa kimataifa ili waweze kufanya
tathmini ya ushirikiano wetu pamoja na namna ya kuendesha majadiliano. Lengo ni
kuboresha ushirikiano wa maendeleo na kushauriana na Serikali juu ya njia nzuri
ya kupokea fedha za nje ili ziweze kuwekezwa kwenye miradi ya maendeleo yenye
kuleta ufanisi zaidi.
4.1.5 Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya
Serikali
67. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa mwaka 2016/17 imepanga pamoja na mambo
mengine kuendelea kuandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali
inayojumuisha matumizi ya kawaida na maendeleo; Kuendelea kupitia mfumo wa
uwasilishaji wa bajeti za Wizara, Idara za Serikali, Mikoa na Halmashauri na
kuhakikisha kuwa Sera na Mipango ya Kitaifa na ile ya Kisekta vyote vimeingizwa
ipasavyo katika Bajeti ya Serikali na kutengewa fedha; Kufanya tathmini ya
Bajeti ya Serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa inazingatia mahitaji ya
makundi yote ya jamii; Kuendelea kuimarisha mifumo ya Kompyuta ya uandaaji
bajeti ili kukidhi mahitaji ya taarifa mbalimbali zinazohitajika na; Kuendelea
kujenga uwezo wa Wizara, Idara za Serikali, Mikoa na Idara katika uandaaji wa
bajeti ya muda wa kati, usimamiaji wake na utoaji taarifa za utekelezaji ikiwa
ni pamoja na ufuatiliaji na tathmini kwa wakati.
4.1.6 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma
68. Mheshimiwa spika, katika mwaka 2016/17 Wizara imepanga kuandaa na kukamilisha Programu ya Usimamizi na udhibiti
wa matumizi ya fedha za umma Awamu ya Tano ya Miaka Mitano 2017/2018 -2021/22;
Kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Serikali wa kada zinazohusiana na
usimamizi wa fedha za umma; Kufanya tathmini ya utekelezaji wa programu kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kupima mafanikio ya utekelezaji wa
Progam ya Awamu ya Nne na; Kusimamia na Kuratibu zoezi la Upimaji wa Mifumo ya
Fedha - Public Expenditure and Financial
Accountability katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
4.1.7 Usimamizi wa Malipo
69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara imepanga kuendelea kutoa
udhamini wa masomo kwa wahasibu, wakaguzi, wagavi na wataalamu wa kompyuta
kutoka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ambao wapo vyuoni; Kusimika Mfumo wa
TISS katika Halmashauri zipatazo 58 zilizopo katika Mikoa ya Dar es Salaam,
Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Morogoro na Dodoma. Wizara imepanga kuendelea
kusimamia, kuimarisha na kuboresha uendeshaji na uunganishaji wa mtandao wa
malipo wa Serikali. Aidha, Wizara imepanga kuunganisha Mfumo wa Malipo wa EFT
katika Wizara ya Fedha na Mipango, Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi; Kuunganisha mfumo wa uwasilishaji mapato wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania - Tanzania Revenue Gateway System (RGS) na mfumo wa Hazina - Treasury
Revenue Accounting System kwa lengo la kupata taarifa za mapato ya kodi kutoka
TRA kielektroniki.
70. Mheshimiwa Spika, Wizara imepanga pia kufuatilia utekelezaji wa Miongozo
ya ukaguzi wa ndani; kukagua mfumo wa kuandaa bajeti; Kufanya ukaguzi maalum
kadri ya mahitaji ya Mlipaji Mkuu wa Serikali na wadau wengine; na kuendelea
kutoa mafunzo na kufanya ufuatiliaji wa miongozo mbalimbali ambayo imetolewa na
Wizara kwa wakaguzi wa ndani wote na wadau mbalimbali wanaotumia miongozo hiyo.
4.1.8 Deni la Taifa
71. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa mwaka 2016/17 imepanga kuendelea kulipa
madeni mbalimbali yaliyokopwa na Serikali ili kugharamia miradi ya maendeleo
nchini pamoja na kuwasilisha michango ya Serikali kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii.
Aidha, kwa kuwa malipo ya fidia kwa wafanyakazi waliokuwa wakipata ajali mahala
pa kazi yalikuwa hayashughulikiwi ipasavyo na waajiri na mifuko iliyopo ya
Hifadhi ya Jamii ambayo mingi ni ya Pensheni, Serikali ilianzisha Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi na Wizara kwa mwaka 2016/17 imepanga kuanza kuwasilisha
mchango wa mwajiri kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ili watumishi wa umma
wakipata ajali mahala pa kazi waweze kulipwa na Mfuko huu kwa wakati.
4.1.9 Usimamizi wa Mali ya Serikali
72. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara chini ya jukumu lake la
kusimamia mali ya Serikali imepanga kufanya uthamini wa ardhi na majengo ili
kuwa na taarifa sahihi za mali ya Serikali; Kuendelea kuondosha mali chakavu,
sinzia na zilizokwisha muda wake; na Kufanya uhakiki wa mali za watu binafsi
zilizo chini ya uangalizi wa Serikali na zile zinazotokana na utaifishwaji kwa
lengo la kuepuka ulipaji wa fidia usiokuwa wa lazima. Aidha, Wizara itahakiki
mali katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali ili kutoa
ushauri wa kupunguza hasara zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi.
4.1.10 Ununuzi wa Umma
73.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka
2016/17 Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini imepanga
kutekeleza yafuatayo: Kufanya mapitio ya kanuni za ununuzi wa umma; Kuandaa
mwongozo wa utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma nchini; Kuwajengea uwezo
wadau mbalimbali wa ununuzi nchini juu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya
Ununuzi wa Umma na kukamilisha tathmini ya ufanisi wa mfumo wa ununuzi wa umma
nchini. Aidha, Wizara imepanga kutekeleza mpango wa mafunzo wa maafisa ununuzi
na ugavi walioko katika Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa
kuwajengea uwezo juu ya usimamizi wa mikataba ya ununuzi; Kutoa mafunzo ya
matumizi ya mfumo wa malipo wa EPICOR 9 kwa baadhi ya maafisa ununuzi na ugavi
Serikalini pamoja na kuendelea kuhakiki taarifa za maafisa ununuzi na ugavi na
kuziweka katika daftari la maafisa ununuzi na ugavi Serikalini.
74.
Mheshimiwa
Spika, kazi nyingine
zilizopangwa kufanywa na Wizara kwa mwaka 2016/17 ni pamoja na kukamilisha
mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao na kuanza kuutumia kwa majaribio kwenye
robo ya pili ya mwaka 2016/17 kwa manunuzi ya madawa na vifaa tiba pamoja na
manunuzi ya bidhaa mtambuka; Kuongeza uwezo wa watumiaji wa Sheria ya Ununuzi
wa Umma kwa kufanya mafunzo kwa wanataaluma
na wadau wengine ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti juu ya taaluma ya ununuzi
na ugavi utakaopelekea kutoa ushauri kwa Serikali kwenye maeneo ya taratibu na
sera za ununuzi na ugavi na; Kuongeza kiwango cha ufaulu wa watahiniwa toka
kiwango cha sasa cha asilimia 42.8 hadi kufikia asilimia 50 kwa kuboresha
mazingira ya kujifunzia.
75.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/17,
Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini imepanga kuendelea na
ununuzi wa magari kwa pamoja; Kuongeza uwezo wa Wakala wa kuhifadhi mafuta
kufikia wastani wa lita 50,000 kila mkoa katika mikoa ya Iringa, Kigoma, Mbeya,
Morogoro na Mwanza; Kuanza ujenzi wa ofisi, ghala na kisima cha mafuta katika
mikoa ya Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Aidha, Wakala wa Huduma ya Ununuzi
Serikalini utaendelea na kazi ya kufunga mfumo wa udhibiti na usimamizi wa
mafuta ya magari na mitambo katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya,
Mwanza, Morogoro, Ruvuma, Singida na Tanga.
4.1.11 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali
76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17
Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imelenga kuendelea kufanya
ukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2015/16.
Ukaguzi utaelekezwa katika ukusanyaji wa mapato na matumizi ya Serikali Kuu,
Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma. Aidha,
ukaguzi utahusisha Sekta ya mafuta na gesi na pia ukaguzi katika sekta ya
madini utaimarishwa. Wizara itaendelea kuimarisha uwezo wa kitaalam kwa
Wakaguzi wake, na kuendelea na ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
ili kuongeza uhuru wa wakaguzi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija
zaidi ili kukidhi matakwa ya viwango vya kimataifa vya taasisi za ukaguzi
pamoja na maazimio ya kimataifa ya Lima na Mexico ambayo Tanzania imeyaridhia.
4.1.12 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma
77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa
Hazina, itaendelea kufanya uhakiki wa
mali za taasisi na mashirika za umma zilizoingizwa katika daftari la mali; Kufuatilia na kuhakiki mali za
mashirika yaliyobinafsishwa ili kubaini mali ambazo hazikuingizwa kwenye
orodha ambazo hivi sasa zinamilikiwa kinyume na sheria ili zirejeshwe
Serikalini; Kufanya utafiti wa taasisi ambazo zina vyanzo binafsi vya mapato
kwa lengo la kuangalia uwezekano wa kuziondoa kwenye utegemezi wa ruzuku ya
Serikali; na kukamilisha maandalizi ya
mfumo wa tathmini na ufuatiliaji
kwa taasisi na mashirika ya umma.
4.1.13 Mafao ya Wastaafu na Mirathi
78. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2016/17 shilingi trilioni 1.14 zimetengwa kwa
ajili ya kulipa mchango wa mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Aidha,
Wizara itaendelea kuboresha kumbukumbu za wastaafu ikiwa ni pamoja na kulipa
pensheni kwa wakati.
4.1.14 Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi
79. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara imepanga kuendelea kupokea
na kuchambua taarifa za miamala shuku zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu
na ufadhili wa ugaidi; Kuendelea kuwasilisha taarifa za intelijensia kwenye
vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi; Kukamilisha
zoezi la kutathmini mianya na viashiria
vya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi nchini; Kuendelea na utekelezaji wa
mikakati ya kitaifa na kimataifa ya udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa
ugaidi; na kuendelea na ukaguzi wa taasisi mbalimbali za fedha na zisizo za
fedha ili kubaini kama sheria na miongozo ya kudhibiti utakasishaji wa fedha
haramu na ufadhili ugaidi inafuatwa ipasavyo.
4.1.15 Tume ya Pamoja ya Fedha
80. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2016/17 Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha
imepanga kuendelea kufanya stadi ya uwekezaji katika mambo ya muungano. Stadi
hii inalenga kubaini ushiriki wa pande mbili za muungano katika uwekezaji kwa
mambo ya muungano. Aidha, Wizara inakusudia kufanya mapitio ya stadi
zilizofanywa na Tume kuhusu mfumo bora wa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa masuala ya fedha yanayohusu mambo ya
muungano.
4.1.16 Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi
81. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizara itaendelea kupokea na
kuchambua miradi ya ubia kwa lengo la kuiidhinisha; Kutoa ushauri kwa Wizara na
Taasisi za Serikali katika kuchagua miradi bora ya ubia; Kuziwezesha taasisi
zenye miradi ya ubia kuajiri washauri elekezi pamoja na kuendelea kutoa elimu
kwa wadau mbalimbali kuhusu sera, sheria na kanuni za miradi ya ubia.
4.2 USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NA MASHIRIKA
YA UMMA CHINI YA WIZARA
82.
Mheshimiwa Spika, mipango na malengo ya bajeti kwa mwaka 2016/17
kwa upande wa mashirika na taasisi za umma zilizochini ya Wizara ni kama
inavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 97 hadi ukurasa
wa 121.
5.0 MAKADIRIO YA MAPATO KWA MWAKA 2016/17
5.1 MAKADIRIO YA MAPATO
83. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara inakadiria kukusanya
maduhuli kiasi cha shilingi 449,699,727,503
kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauzo ya nyaraka za zabuni,
kodi za pango, mauzo ya leseni za minada
na mishahara isiyolipwa, gawio, marejesho ya mikopo na michango kutoka katika
Taasisi na Mashirika ya Umma.
5.2 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2016/17
84. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha
na Mipango kwa mwaka 2016/17 kupitia mafungu yote tisa ya kibajeti inaomba
kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 8,716,493,400,510 (bilioni 8,716.49) kwa
ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya
fedha hizo, Shilingi 45,454,478,000 (bilioni 45.45) ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 8,671,038,922,510
(bilioni 8,671.04) ni kwa ajili ya
Matumizi Mengineyo. Kwa upande wa fedha
za maendeleo, Wizara ya Fedha na Mipango inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 791,998,424,268 (bilioni 791.99).
Kati ya fedha hizo, Shilingi 723,150,000,000 (bilioni 723.15) ni Fedha za Ndani na Shilingi 68,848,424,268 (bilioni 68.85) ni Fedha za Nje.
Mchanganuo kwa kila fungu ni kama ifuatavyo:-
5.2.1 FUNGU 50 – WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
85. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya
kawaida - Shilingi 50,716,878,000 (bilioni 50.72). Kati ya
hizo:
(i) Mishahara - Shilingi 6,984,801,000 (bilioni 6.98)
(ii) Matumizi Mengineyo – Shilingi 43,732,077,000 (bilioni
43.73)
(b) Miradi ya Maendeleo - Shilingi 26,035,591,500 (bilioni 26.03). Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani - Shilingi 9,000,000,000 (bilioni
9.00).
(ii) Fedha za Nje - Shilingi 17,035,591,500 (bilioni 17.03).
5.2.2 FUNGU 21 – HAZINA
86. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya
Kawaida - Shilingi 411,279,240,510 (bilioni 411.28). Kati ya
hizo:
(i) Mishahara ya fungu hili - Shilingi 4,474,752,000 (bilioni 4.47).
(ii) Matumizi
Mengineyo - Shilingi 406,804,488,510
(bilioni 406.8) ambazo ni kwa ajili
ya matumizi ya Idara, Taasisi zilizo chini ya Fungu hili, pamoja na matumizi
maalum.
(b) Miradi ya
maendeleo - Shilingi
740,155,523,400 (bilioni 740.15).
Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani - Shilingi 699,500,000,000 (bilioni 699.5)
(ii) Fedha za Nje - Shilingi 40,655,523,400 (bilioni 40.65)
5.2.3 FUNGU 22- DENI LA TAIFA
87. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)
Matumizi
ya Kawaida - Shilingi 8,009,341,187,000
(bilioni 8,009.34).
Kati ya hizo:
(i) Mishahara - Shilingi 9,340,716,000 (bilioni
9.34)
(ii) Matumizi
Mengineyo - Shilingi 8,000,000,471,000
(bilioni 8,000)
5.2.4 FUNGU 23 – MHASIBU MKUU WA SERIKALI
88. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya
Kawaida - Shilingi 45,585,865,000 (bilioni 45.58). Kati ya hizo
(i) Mishahara - Shilingi 6,784,116,000 (bilioni
6.78)
(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi 38,801,749,000 (bilioni 38.8).
(b) Miradi ya
Maendeleo – Shilingi 4,493,750,000
(bilioni 4.49). Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani - Shilingi 2,000,000,000 (bilioni 2).
(ii) Fedha za Nje - Shilingi
2,493,750,000 (bilioni 2.49).
5.2.5 FUNGU 7 – OFISI YA MSAJILI WA HAZINA
89. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)
Matumizi
ya Kawaida – Shilingi
160,181,000,000 (bilioni 160.18). Kati
ya hizo:-
(i) Mishahara - Shilingi 1,974,355,000 (bilioni 1.97)
(ii) Matumizi
Mengineyo - Shilingi 158,206,645,000
(bilioni 158.21).
(b) Miradi ya
Maendeleo – Shilingi 3,228,540,000
(bilioni 3.23) Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani – Shilingi 650,000,000 (bilioni 0.65).
(ii) Fedha za
Nje -Shilingi 2,578,540,000 (bilioni 2.58).
5.2.6 FUNGU 10 – TUME YA PAMOJA YA FEDHA
90. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya Kawaida - Shilingi 1,374,270,000 (bilioni 1.37).
Kati ya hizo:-
(i) Mishahara - Shilingi 464,472,000 (bilioni 0.46)
(ii) Matumizi Mengineyo- Shilingi 909,798,000 (bilioni 0.91).
5.2.7 FUNGU 13 – KITENGO CHA UDHIBITI WA FEDHA HARAMU
91. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kwa Matumizi ya Kawaida - Shilingi 1,603,081,000 (bilioni
1.6).
5.2.8 FUNGU 45 – OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI
92. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)
Matumizi
ya Kawaida Shilingi 32,373,096,000
(bilioni 32.37). Kati ya hizo:-
(i) Mishahara ni Shilingi
13,870,774,000 (bilioni 13.87)
(ii) Matumizi Mengineyo ni
Shilingi 18,502,322,000 (bilioni 18.50)
(b)
Miradi
ya Maendeleo Fedha za Nje ni Shilingi 12,285,427,368 (bilioni 12.28).
(i) Fedha za Ndani – Shilingi
8,000,000,000 (bilioni 8.00)
(ii) Fedha za Nje – Shilingi 4,285,427,368 (bilioni 4.28)
5.2.9 FUNGU 66 – TUME YA MIPANGO
93. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya
kawaida - Shilingi 4,038,783,000
(bilioni 4.04). Kati ya hizo:
(i) Mishahara - Shilingi 1,560,492,000 (bilioni
1.56)
(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi 2,478,291,000 (bilioni 2.48)
(b) Miradi ya
Maendeleo – Shilingi 5,799,592,000
(bilioni 5.79). Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani - Shilingi 4,000,000,000 (bilioni 4).
(ii) Fedha za
Nje - Shilingi 1,799,592,000 (bilioni
1.79).
94. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu maombi
ya fedha kwa mafungu Tisa niliyoyataja katika aya ya 190 ya kitabu cha hotuba
yangu, nichukue fursa hii pia kuwasilisha maombi ya fedha kwa mwaka 2016/17 kwa
ajili ya Mfuko wa Mahakama (Fungu 40) na Mfuko wa Bunge (Fungu 42). Maombi haya
ni kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanyika kwenye kifungu cha 59 kifungu kidogo
cha 3 cha Sheria ya Utawala wa Mahakama Sura 237 na kifungu cha 29 kifungu
kidogo cha 3 cha Sheria ya Utawala wa Bunge, Sura 115, kupitia Sheria ya Bajeti
ya mwaka 2015. Sheria hizi zinampa mamlaka Waziri mwenye dhamana na masuala ya
fedha kuwasilisha Bungeni maombi ya fedha za matumizi ya mifuko hii.
95. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sheria hii, naomba Bunge lako Tukufu
liidhinishe jumla ya Shilingi 230,693,160,000 (bilioni 230.69) kwa
ajili ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo kwa mafungu haya mawili. Kati ya hizo, Shilingi 176,931,426,000
(bilioni 176.93) ni kwa ajili ya
Matumizi ya Kawaida na Shilingi 53,761,734,000 (bilioni
53.76) ni kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.
Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo:-
5.2.10 FUNGU 40 – MFUKO WA MAHAKAMA
96.
Mheshimiwa
Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 84,865,309,000 (bilioni 84.86). Kati ya hizo:
(i) Mishahara - Shilingi 50,345,775,000 (bilioni 50.35)
(ii) Matumizi
Mengineyo – Shilingi 34,519,534,000
(bilioni 34.52)
(b) Miradi ya Maendeleo - Shilingi 46,761,734,000 (bilioni 46.76). Kati ya hizo:
(i) Fedha za
Ndani - Shilingi 24,000,000,000 (bilioni 24.00).
(ii) Fedha za Nje
- Shilingi 22,761,734,000 (bilioni 22.76).
5.2.1 FUNGU 42 – MFUKO WA BUNGE
97.
Mheshimiwa
Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2016/17, Wizara inaomba
kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 92,066,117,000 (bilioni 92.07). Kati ya
hizo:
(i) Mishahara - Shilingi 23,798,609,000 (bilioni 23.80)
(ii) Matumizi
Mengineyo - Shilingi 68,267,508,000
(bilioni 68.27)
(b) Miradi ya Maendeleo Fedha za Ndani - Shilingi
7,000,000,000 (bilioni 7.00
6.0 SHUKRAN
98.
Mheshimiwa Spika,
naomba nitumie nafasi hii kuzishukuru nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa
ambayo kwa namna moja ama nyingine yamesaidia katika utekelezaji wa bajeti ya
Wizara. Kwanza napenda kuzishukuru nchi za Finland, Uingereza kupitia shirika
la DFID, Canada, Denmark kupitia shirika la DANIDA, Ireland, Japan kupitia
shirika la JICA, Marekani, Norway, Sweden, Uholanzi na Ujerumani. Pia taasisi
mbalimbali za kimataifa ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia,
Global Fund, Umoja wa Ulaya, na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNFPA na UNDP.
99.
Mheshimiwa Spika, napenda
pia kuwashukuru sana wafanyakazi na wananchi wote ambao wameendelea kulipa kodi
kwa hiari na pia kushiriki katika ujenzi wa Taifa letu. Ni imani yangu kuwa
juhudi hizi zinazochukuliwa na Serikali yetu na wananchi zitatuwezesha kufikia
malengo yetu ya kukuza uchumi na kupambana na umaskini.
100.
Mheshimiwa Spika, mwisho
kabisa napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba
hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz).
101. Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa hoja.

No comments:
Post a Comment