Mafundi wakiendelea na upakaji rangi katika banda la CRDB katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar e Salaam.
Afisa Habari Idara ya Habari,MAELEZO Bi.Immaculate Makilika akizungumza jambo na Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw.Baruti Mwaigaga (kushoto) katika banda la Wizara hiyo viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha African Flowerless fashion cha Arusha kinachouza bidhaa zake nje ya nchi. Kulia ni Afisa wa kikundi hicho Bi.Suzana Mwalongo.
Fundi akipaka rangi kwenye uwanja wa moja ya banda katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa kwa ajili ya maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza rami jana.
Askari
wa JKT pamoja na FFU wakihakikisha usalama wakati wananchi wakiingia katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere kuangalia bidhaa mbalimbali baada ya maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, yalianza rami jana, jijini Dar es Salaam.
Na Immaculate Makilika- MAELEZO, tarehe 29/06/2016 Dar es Salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu
wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji
wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Afisa Biashara wa
Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja vya Mwl
Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza jana jijini Dar es Salaam.
“Kufuatia kuwepo kwa tatizo kubwa la
upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda hapa nchini,
Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa taarifa zinazohusu upatikanaji wa
mikopo ili kusaidia wananchi, kitu ambacho hakikuwepo awali” alisema Bw.
Mwaigaga
Alisema lengo la mkakati huo ni
kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha kiwanda kupata taarifa sahihi
ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kupata mkopo ambao unaondoa usumbufu kwa
walengwa ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mikakati mingine ya Serikali katika
kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na kuanzisha programu ya kuendeleza
viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya Ruvuma, Pwani, Iringa, Tanga na Manyara.
Naye,
Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika kutekeleza
azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Wizara
inawaunganisha wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na kuwapatia
masoko ya mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya Oramu pamoja na
Murza Mills.
Aidha,
wananchi wamesisitizwa kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara
pamoja na taasisi zake za BRELA, TBS, TFDA , CBE na SIDO lililopo katika
viwanja hivyo vya maonesho ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu namna za
kufanya biashara pamoja na kuanzisha viwanda nchini.







No comments:
Post a Comment