Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)na vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Maelezo)
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
imetoa utabiri wa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti
mwaka huu.
Akizungumzia kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu,
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia
kuwa na hali
ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa
kujitokeza katika maeneo machache hususanya ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda
wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na Pemba).
Katika
kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa
makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto
la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa
nchi.
Hata hivyo,katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu
maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani.
Aidha, izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi
mapema asubuhi. “Aliendelea
kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja
na kupungua kwa joto la bahari
katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la
baharà katikaeneo la magharibi wa bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni
hadi Agosti 2016”.
Aidha, joto katika bahari ya
Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha
upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki hususankatika maeneo ya
Ukanda wa Ziwa Viktoria. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika
eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa
kusi.
Kwa upande mwengine, Afisa
Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa
hususan za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya
habari, tovuti ya Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi
karibuni TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo
kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa na nchi
kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na maziwa kuchukua
hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.
Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbalipamoja
na Taasisi, Mamlaka za Serikali na jamii kwa ujumla kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika kipindi
chamsimu wa mvua za Masika 2016 kwa
kutumia Taarifa, Agalizona Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni
wazi kuwa kwa hatua hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na
hivyo kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za
kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.
Kwa tarifa ya kina kuhusiana na
mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu.
IMETOLEWA
NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA



No comments:
Post a Comment