TANGAZO


Friday, May 27, 2016

WAZIRI PROFESA MBARAWA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE, KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO

Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji. (Picha zote na Beatrice Lyimo)
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. 
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es Salaam. 
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto  kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali. 
Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto  kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali. 
Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.

Na Betrice Lyimo-MAELEZO
27/05/2016
Dar es Salaam
SERIKALI kwa kushirikiana na Kampuni ya   Mabey Bridge ya nchini Uingereza wamejipanga kikamilifu kujenga  barabara tatu za juu (Fly Overs) na  barabara nne   za watembea  kwa lengo la kupunguza  msongamano wa  foleni jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa  Makame Mbarawa wakati wa mazungumzo hayo na  kampuni ya   Mabey  Bridge  ya Uingereza  kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo nchini.

Profesa Mbarawa alisema kuwa barabara hizo  zitajengwa hasa maeneo ambayo yana msongamano  mkubwa  wa magari  ikiwa  ni pamoja na  eneo la barabara ya Mwenge.

“Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha  wananchi  wanakuwa na miundombinu iliyobora  hasa katika  upande wa  barabara za magari na barabara za waenda kwa miguu ili kuwarahisishia wananchi  kuwahi kuwajibika katika maeneo yao ya kazi”. 

Mbali na hayo,  Waziri Mbarawa alifanya ziara ya kushtukiza  katika Daraja la  Nyerere lililopo maeneo ya  Kigamboni kwa  lengo la kutaka kujua maendeleo ya daraja hilo na  kumtaka msimamizi wa  daraja hilo kuandaa kadi maalumu au kitambulisho  zitakazotumika kwa lengo la kupunguza msongamano  wakati wa kulipia tozo.

vilevile Waziri aliwataka  wananchi  kuwa waangalifu na miundombinu ya   daraja hilo  na  endapo  kuna mtu  atakaye bainika  kuharibu   atachukuliwa  hatua kali za kisheria ikiwa  ni pamoja  na  kulipa faini za gharama ya juu.

“kuanzia sasa  kunatakiwa kuwepo na  faini kali  kwa mtu yeyote atakaye haribu  miundombinu ya daraja  hili kwa lengo la kulifanya daraja   lidumi kwa muda mrefu” alisisitiza Waziri Mbarawa.
 
Kwa upande wake  Msimamizi   Mkuu  wa daraja la Nyerere, Gerald  Sondo  alisema   wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya madereva wa  daladala kushindwa kutumia daraja hilo na  kudai kuwa tozo ni kubwa.

Vilevile  Waziri huyo alifanya ziara  katika eneo la ujenzi wa  mtambo wa Mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki (Flow Meter)  kuona maendeleo ya ukarabati wa mtambo hio uliyoharibika hivi karibuni kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kumtaka mkandarasi  kuhakikisha  eneo hilo linazungishiwa   ukuta  ili kuziba  mitambo  hiyo.

No comments:

Post a Comment