TANGAZO


Friday, May 13, 2016

Walalamika kuugua kutokana na uchimbaji


Image captionWachimbaji hao wamelalamika kwa muda mrefu kutaka kulipwa
Wachimbaji wa zamani wa madini ya dhahabu Afrika kusini sasa wanaweza kuendelea kuwasilisha kesi dhidi ya makampuni ya madini kuhusu athari ya afya inayosemekana kutokana na kazi waliokuwa wakifanya, mahakama ya Johannesburg imeamua.
Umauzi wa mahakama ya juu unatoa nafasi kwa kitakachokuwa kesi inayowawakilisha wachimbaji hao iliyo kubwa katika historia ya Afrika kusini.
Wachimbaji hao wa zamani wanasema wameathrika kwa ugonjwa wa mapafu usio tibika - silicosis, kutokana na kufanya kazi kwa miaka mingi katika migodi.
Mahakama hiyo inasema kesi hiyo inayowawakilisha ndio "hatua pekee iliyo sawa".
Uamuzi wa Jaji Phineas Mojapelo huedna ukasabaisha kesi itakayodumu kwa hadi miaka 10, mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anaarifu kutoka Johannesburg.
Lakini wachimbaji hao wa zamani wanatumai kwamba huedna kesi hiyo ikasaida kuimarisha maisha yao pamoja na ya familia zao, anasema mwandishi wetu.
Silicosis, husababishwa klwa kupumua vumbi la silica linalopatikana katika mawe ya dhahabu na inaweza kusababisha matatizo ya kupumua, kukohoa kwa muda mrefu na maumivu ya kifua na pia inaweza kusabisha kifua kikuu.

No comments:

Post a Comment