Mtaalam wa TEHAMA katika moja ya Ofisi za Serikali akiwa kazini.
Na Aron Msigwa – Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka taasisi zote
zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki
ya intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti kuzitumia simu
hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza
gharama za mawasiliano Serikalini.
Meneja Habari, Elimu
na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili kuziwezesha taasisi za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama na kupunguza gharama za mawasiliano.
Amesema kuwa Serikali kupitia
Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha taasisi
za Serikali 72 ambazo
zinajumuisha Wizara, Idara zina zojitegemeana na Wakala za Serikali
na kuongeza kuwa taasisi hizo zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani ‘Government Communication Network
(Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya
kazi kwa ufanisi.
“Kupitia mfumo wa simu hizi
zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa taasisi iliyounganishwa anaweza kupiga
simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga
simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja”
Amesema Bi. Suzan.
Aidha, amesema
Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa kuwa, taasisi hizo zitaweza
kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama
na uhakika. Pia simu hizo zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya
mkutano kwa njia ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na
gharama za usafiri.
Hata hivyo
amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa Seikali zitaendelea
kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo kwa kupitia mtoa huduma wa simu
za mezani (PSTN Provider) kama vile TTCL.
No comments:
Post a Comment