TANGAZO


Sunday, May 8, 2016

SIMBA YAKUBALI KICHAPO CHA BAO 1-0 KUTOKA KWA MWADUI FC LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa matangazo ukionesha Simba 0 Mwadui FC bao 1.  
Mchezaji Mohamed Hussein wa Simba akipiga krosi huku akifuatwa na Malika Ndeule wa Mwadui FC.
Hamis Kiiza wa Simba akidondoka huku Razak Khalfan wa Mwadui FC akiukimbilia mpira.  
Malika Ndeule wa Mwadui FC akiruka juu kuuwahi mpira huku akifuatwa na Mohamed Hussein wa Simba. 
Abdallah Mfuko wa Mwadui FC akiutuliza mpira kifuani huku akizongwa na Peter Mwalyanzi wa Simba. 
Said Hamisi Juma wa Simba akipasua katikati ya wachezaji wa Mwadui FC, Razak Khalfan (8) na David Luhende. 
Said Hamisi Juma wa Simba akiwatoka wachezaji wa Mwadui FC, Razak Khalfan (kushoto) na David Luhende.  
Brian Majegwa wa Simba akipiga mpira huku akifuatwa na Malika Ndeule wa Mwadui FC. 
Mussa Mgosi wa Simba akiwatoka wachezaji wa Mwadui FC.
Hapa golikipa Shaaba Kado wa Mwadui FC akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kudondoka zikiwa zimesalia dakika 3 za nyongeza wakati matokeo yakionesha Simba 0 na Mwadui bao 1. 
Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ukionesha Simba 0 Mwadui FC bao 1.  

No comments:

Post a Comment