Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi akizungumza na vijana na wadau wa vijana (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana na wadau wa vijana akifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana Jijini Dar es Salaam.
Vijana wanaoishi kwa matumaini wakitoa nasaha kwa vijana wengine jinsi ya kujitunza na kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kilimanjaro marathoni changia dola elfu tano kuondoa unyanyapaa, maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na vifo vitokanavyo na ukimwi Bw. Mrisho Mpoto akiteta jambo na vijana jinsi ya kupambana na VVU jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Dkt. Abdallah Possi (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na
vijana walioshiriki katika mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya
vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana jana jijini Dar es Salaam. Wanne
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho.
Na Genofeva Matemu – Maelezo
Tarehe 18/05/2016
SERIKALI imedhamiria
kuhakikisha kuwa vijana wote nchini wanashirikishwa kikamilifu na kupatiwa
huduma zinazotakiwa ili kumaliza uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya
ukimwi, kupunguza ubaguzi na unyanyapaa unaotokana na ukimwi pamoja na
kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Dkt. Abdallah Possi alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa
masuala ya vijana jana jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Possi amesema kuwa asilimia 2 ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yapo
miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa
vijana wa kike uko juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa
miaka 23 hadi 24.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi Fatma
Mrisho amesema kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa
watoto na vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo
kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI.
“Vijana
ni nguvu kazi ya taifa la leo, wakipatiwa nafasi ya kujitambua na kuwasilisha
hisia zao utegemezi ndani yao utapungua, ni vyema vijana wakaandaliwa mazingira
ambayo watakua huru kushiriki katika masuala ya VVU na UKIMWI” Alisema Bibi.
Mrisho.
Aidha
Bibi. Mshiro amemtaka kila kijana aliyeshiriki mkutano huo kubeba mambo muhimu manne
na kuwafikishia vijana wengine kumi waliopo vijiweni, maofisini ama sehemu
nyingine yeyote ile ili kuweza kusambaza elimu waliyoipata kwa kila kijana nchi
nzima na kuokoa afya za vijana wenzao.
Kwa upande wake
kijana anayeishi kwa matumaini Bi. Wittiness Nakanje ameiomba serikali
kuanzisha kliniki maalumu za vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuwaweka vijana
kuwa huru kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.
Kulingana
na utafiti wa viashiria vya UKIMWI kwa mwaka 2011/2012 tanzania inajumla ya vijana
milioni 12 wa umri wa 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni 16 wa umri wa
miaka 19 hadi 24 ikiwa ni asilimia 24 ya Watanzania wapatao milioni 44, idadi
hiyo ya vijana inajumuisha wasichana wapatao 7,430,840 na wavulana 6,924,612.
Kwa
mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 vijana wa umri wa miaka 19 hadi
24 wako 3, 954,039 ambapo wasichana
idadi yao ni 2,160,986 sawa na asilimia 55 na wavulana 1,793,053 sawa na
asilimia 45.









No comments:
Post a Comment