TANGAZO


Saturday, May 28, 2016

Mkutano wa Trump wakabiliwa na ghasia

Image copyrightREUTERS
Image captionMkutano wa Trump wakumbwa na ghasia
Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Marekani walitumwa kwenye mji wa San Diego, jimbo la California, kuzuia makabiliano kati ya maelfu ya wafuasi na wanaompinga mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump.
Waandamanji hao walipeperusha bendera za Marekani na Mexico, wakati bwana Trump akitoa hotuba yake.
San Diego, ni kilomita chache tu kutoka mpaka wa Mexico na Marekani.
Image copyrightAFP
Image captionMkutano wa Trump mjini San Diego
Bw Trump amesisitiza kuwa iwapo atachaguliwa kuliongoza taifa hilo, atajenga ukuta mkubwa ili kuwazuia wahamiaji haramu kuingia nchini humo

No comments:

Post a Comment