TANGAZO


Saturday, May 28, 2016

Cantona amlaumu Deschamps kwa ubaguzi

Image captionEric Cantona
Wakili wa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa atamshtaki Eric Cantona kwa kusema kuwa kikosi chake cha Euro 2016 kilichaguliwa kwa ubaguzi.
Cantona alisema siku ya Alhamisi kwamba Deschamps aliwawacha kwa makusudi wachezaji wawili wenye mizizi yao Afrika, Karim Benzema na Hatem ben Arfa nje ya kikosi hicho.
''Benzema ni mchezaji mzuri'', ''Ben Arfa pia ni mchezaji mzuri'', aliambia gazeti la the Guradian. Lakini Deschamps, ana jina la Kifaransa.
''Pengine ni yeye pekee nchini Ufaransa ambaye ana jina la Kifaransa''. Aliendelea kusema: ''Ben Arfa pengine ndio mechezaji bora Ufaransa leo. lakini wana mizizi yao''.
Image copyrightAFP
Image captionKocha wa kikosi cha Ufaransa
Ninarahusiwa kufikiria kuhusu hilo.
Akizungumza na gazeti la michezo L'Equipe, wakili wa Deschamps ameyataja matamshi hayo kama yasio kubalika, ya kumuharibia jina na kwamba mteja wake atakwenda mahakamani.

No comments:

Post a Comment