Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew akiwaeleza waandishi wa Habari leo
Jijini Dar es salaam kuhusu kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi
kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA hali iliyochangia kuongeza tija
kupitia kituo cha huduma kwa mteja kilichopo Makao Makuu ya Wizara hiyo na Katika
Ofisi zote za Kanda.kushoto ni Msajili
wa Hati Msaidizi
Msajili wa Hati Msaidizi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Apollo Laizer akitoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na kanuni wanapotaka kumiliki Ardhi ili kuepusha migogoro ya Ardhi. Kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu maboresho katika kuwahudumia wananchi kupitia kituo cha huduma kwa mteja.

Frank
Mvungi-Maelezo
WIZARA ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi imehudumia wananchi 41,932 kati
ya Novemba, 2015 hadi sasa kupitia
Kituo cha Huduma kwa Mteja.
Kauli hiyo
imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamishina wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathanael
Methew wakati wa mkutano na vyombo vya habari, uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO),
ambapo alisema lengo la kituo hicho ni
kuongeza tija na kasi ya kuwahudumia wananchi.
Naye Msajili
wa hati msaidizi Bw.Apollo Laizer alitoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na
kanuni wanapotaka kumiliki ardhi ili kuepuka migogoro inayohusu sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment