Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George Simbachawene (kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR Tamisemi), Selemani Jaffo.
Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Lwekatare akitoa taarifa ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George
Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi),
Selemani Jaffo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Msajili Masaidizi wa Hazina Jones Mwalemba akitoa ufafanuzi namna ofisi yake inavyochangia katika kukamilisha mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Na EleuteriMangi-MAELEZO
WAZIRI wa NchiOfisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene amewaagiza
wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi
huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri
Simbachawene unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi
31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili kuhakikisha wanatoa
huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri
mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema
iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi
sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za mradi huo na
kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya majaribio angalau yafike
15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya
kukamilisha mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo
haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi walizojipangia
na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia taarifa kila baada ya
siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa
wa kazi wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi huo
imekamilika na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo waitunze miundombinu
hiyo ikiwemo barabara na vifaa vitakavyokuwa vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya
DART ni kulihujumu taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao
ili mradi uwe wa tija kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji
wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya
wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau
wa mradi wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake Selemani
Jaffo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo
haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi kupitia
eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140
ambayo yanatarajiwa kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es Salaam.









No comments:
Post a Comment