Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na uongozi wa Mkoa wa Kagera baada ya kuwasili
mkoani hapo akiwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za Wizara,
kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia
vitendea kazi Maafisa Mawasiliano
wa mkoa huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Kagera
kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za Wizara,
kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia
vitendea kazi Maafisa mawasiliano
wa mkoa huo. Wengine pichani ni Mkuu wa
wilaya ya Bukoba Bw. Jackson Msome na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Adam
Mohamed Swai.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akikabidhi Tablet tano
kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bw. Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya Maafisa Habari wa Mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Jackson Msome ambaye
anamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu
akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa ziara ya waziri
huyo katika mkoa huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akizungumza jambo na waandishi wa habari wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya
ujenzi wa Uwanja wa Kaitaba. Uwanja huo umeshawekwa nyasi za bandia na maboresho
mengine yanaendelea.

No comments:
Post a Comment