Msafara wa wawekezaji kutoka Oman, ukiwasili kwenye Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, kuangalia fursa za uwekezaji, mkoani Pwani juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wawekezaji kutoka Oman, wakielekea Ofisi za Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, mkoani Pwani mara baada ya kuwasili kwenye ranchi hiyo juzi.
Wawekezaji kutoka Oman wakipokewa na kusalimiana na Meneja wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Dk. James Mtae (kulia), waliofika kuangalia fursa za uwekezaji, mkoani Pwani juzi.
Meneja wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Dk. James Mtae (kulia), akizungumza na wawekezaji kutoka Oman, walipofika kwenye ranchi hiyo juzi kuangalia fursa za uwekezaji.
Meneja wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Dk. James Mtae (wa pili kulia), akiwaonesha eneo la ranchi hiyo, wawekezaji hao kutoka Oman, waliofika nchini kuangalia fursa za uwekezaji, mkoani humo juzi.
Baadhi ya wawekezaji kutoka Oman, wakiangalia sehemu mbalimbali za ranchi wakati wa ziara hiyo.
Baadhi ya mifugo iliyomo kwenye ranchi ya Ruvu ikiwa katika malisho.
Baadhi ya wawekezaji hao kutoka Oman, wakiangalia ng'ombe waliomo kwenye ranchi hiyo.
Baadhi ya wawekezaji hao kutoka Oman, wakitembelea sehemu mbalimbali za ranchi hiyo.
Baadhi ya kondoo waliomo kwenye ranchi hiyo, wakiwa kwenye malisho.
Mmoja wa wawekezaji hao kutoka Oman, akiangalia jinsi nyama inavyokatwa kwenye bucha la ranchi hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Dk. James Mtae, akiwaonesha eneo la machinjio ya kisasa yaliyowekwa jiwe la msingi tokea mwaka 2010 na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete ambayo yametelekezwa bila kuendelezwa hadi leo.
Jiwe la msingi lililowekwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010.
Meneja wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Dk. James Mtae, akiwaonesha wawekezaji kutoka Oman jiwe la msingi la machinjio ya kisasa lililowekwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Wawekezaji wakiangalia magofu ya majengo yaliyotelekezwa yaliyokuwa yawe machinjio ya kisasa walipotembelea eneo hilo juzi.
Wawekezaji kutoka Oman, wakiwasili kwenye Mkahawa wa JKT Ruvu kupata chakula cha mchana.
Wawekezaji kutoka Oman, wakipata vinywaji kupoza makoo yao baada ya kutembelea ranchi ya Ruvu na magofu ya majengo ya machinjio ya kisasa mkoani Pwani juzi.
Wawekezaji kutoka Oman, wakipata chakula kwenye mgahawa huo.
Wawekezaji kutoka Oman, wakipata picha ya pamoja baada ya kupata chakula na kuagana na uongozi wa ranchi hiyo.
Wawekezaji kutoka Oman, wakipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kusindika nyma Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara hiyo.
Wawekezaji kutoka Oman, wakipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kusindika nyama cha Kampuni ya Frostan Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara hiyo.
Wawekezaji kutoka Oman, wakiondoka kwenye kiwanda hicho.

No comments:
Post a Comment