TANGAZO


Tuesday, April 19, 2016

WATEJA WANNE STARTIMES KWENDA KUSHUHUDIA FAINALI COPA ITALIA JIJINI ROMA

Afisa Msadizi wa Uhusiano wa Umma wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchezeshwa moja kwa moja kwa droo ya kuwapata washindi wawili wa kwenda kutazama fainali za kombe la Italia au Copa Italia baina ya timu za AC Milan na Juventus mnamo mwezi Mei 21, 2016 katika jiji la Roma, nchini Italia. Droo hiyo ilichezeshwa moja kwa moja kutoka Makao Makuu ya kampuni hiyo yaliyoko jijini Beijing, China kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. 
Afisa Msadizi wa Uhusiano wa Umma wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchezeshwa moja kwa moja kwa droo ya kuwapata washindi wawili wa kwenda kutazama fainali za kombe la Italia au Copa Italia baina ya timu za AC Milan na Juventus mnamo mwezi Mei 21, 2016 katika jiji la Roma, nchini Italia. Droo hiyo ilichezeshwa moja kwa moja kutoka Makao Makuu ya kampuni hiyo, yaliyoko jijini Beijing, China kupitia chaneli ya StarTimes Swahili.  
Afisa Msadizi wa Uhusiano wa Umma na Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey (kushoto) na Bw. Damien Li (kulia) wakizungumza na mshindi wa kwenda kutazama fainali za kombe la Italia au Copa Italia baina ya timu za AC Milan na Juventus mnamo mwezi Mei 21, 2016 katika jiji la Roma, nchini Italia. Mshindi huyo alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo moja kwa moja kutoka makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko jijini Beijing, China kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. 
Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchezeshwa moja kwa moja kwa droo ya kuwapata washindi wawili wa kwenda kutazama fainali za kombe la Italia au Copa Italia baina ya timu za AC Milan na Juventus mnamo mwezi Mei 21, 2016 katika jiji la Roma, nchini Italia. Droo hiyo ilichezeshwa moja kwa moja kutoka makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko jijini Beijing, China kupitia chaneli ya StarTimes Swahili.

Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam; April 19, 2016
WATEJA wanne wa Kampuni ya StarTimes Tanzania wamejipatia fursa ya kwenda kushuhudia fainali za kombe la Italia almaarufu kama Copa Italia kati ya timu ya AC Milan na Juventus mnamo tarehe 21 mwezi Mei mwaka huu mjini Roma, Italia kupitia droo ya moja kwa moja iliyochezeshwa kupitia chaneli ya StarTimes Swahili kutoka makao makuu ya kampuni jijini Beijing, China juzi.

Akizungumza baada ya droo ya kuwapata washindi hao Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li amebainisha kuwa washindi wa leo wawili wamepatikana na kukamilisha idadi ya washindi wanne ambapo wawili walipatikana wiki iliyopita.

“Droo ya leo imetupatia washindi wawili ambao wote ni wakazi wa jijini Dar es Salaam, wa kwanza alikuwa ni Bi. Augusta John mkazi wa Magereza Keko, Temeke na wa pili ni Bi. Rehema Dauda, mkazi wa Tank Bovu, Mbezi Beach Kinondoni. Washindi hawa wataungana na wenzao wanne ambao watajumuika pamoja kwa safari ya kwenda Italia na kushuhudia fainali ya kombe la Copa Italia mwezi ujao, ambapo watalipiwa kila kitu na kampuni ya StarTimes.” Alisema Bw. Li

Meneja huyo wa masoko alifafanua kuwa washindi hawa wanne wamepatikana kwa njia mbili tofauti, “Washindi wawili waliopatikana wiki iliyopita walipatikana baada ya kutakiwa na kampuni kujipiga ‘selfie’ wakiwa wanatazama chaneli ya StarTimes Swahili wakati alama ya mpira ikiwa na nembo ya kampuni kutokea na kisha ku-tag akaunti yake ikiwa na hiyo picha na ya kampuni. Na wawili waliopatikana leo ni miongoni mwa wateja ambao walitakiwa kulipia kifurushi kisichopungua shilingi 10,000/-“

“Lengo kubwa la kuwazawadia nafasi hii wateja wetu kwenda Italia kushuhudia mechi hizo ni kutaka kuwapa hamasa zaidi kwao kutazama na kufurahia vipindi na chaneli zetu za michezo. Pia kuwadhihirishia kuwa sisi tunafanya kila liwezekanalo kuzidi kuwaletea mechi nyingi zaidi. Na hii si mara ya kwanza kwa kuwapatia fursa wateja wetu kwenda kushuhudia mechi live huko Ulaya, kwani tayari kuna washindi wamekwishapatikana kwenda kutazama mechi za ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili.” Alihitimisha Bw. Li

Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kutangazwa mshindi, Bi. Rehema Dauda mkazi wa Tank Bovu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam alifafanua furaha yake ya kubahatika kupata fursa ya safari hiyo ya kwenda Ulaya kuangalia mechi moja kwa moja.

“Nimefurahi sana, nimeshangazwa pia na fursa hii kwani sikuitegemea na ni kitu kizuri kwa kampuni ya StarTimes kuwajali wateja wake kwa namna hii. Mimi niko tayari kwenda kwa safari hiyo ili mradi kwamba nimehakikishiwa kuwa kila kitu kitagharamiwa na wao, sidhani kama ni kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukataa,” alifafanua Bi. Dauda na kumalizia, “Nimekuwa ni mteja wa huduma za StarTimes kwa muda mrefu na nafikiri haya ni matunda yake leo. Ningependa kutoa wito kwa wateja wengine kuchangamkia fursa kama hizi na pia kwa kampuni kuendelea kuboresha huduma zao ili sisi wateja kuzidi kunufaika na kuendelea kuwaunga mkono.”

Naye kwa upande wake Afisa Msaidizi wa Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Kijanga Geofrey aliongezea kwa kusema kuwa, “Mechi za michuano ya kombe la Italia au Copa Italia yote ilikuwa ikirushwa ndani ya chaneli za StarTimes kama vile Sport Life, Sport Premium, World Football na Sport Arena. Wateja wetu waliweza kushuhudia mechi zote moja kwa moja mpaka kufikia hatua ya mwisho iliyobakia ambapo timu za AC Milan na Juventus kufanikiwa kutinga fainali.”

“Hivyo basi hii ni fursa kubwa kwa wateja kwenda kushuhudia fainali hiyo itakayozikutanisha timu kubwa na zenye historia barani Ulaya na Duniani kwa ujumla zikiwa na wachezaji nyota wengi kama vile Paul Pogba, Alvaro Morata, Mario Mandzukic, Buffon, Paul Dibala (kwa upande wa Juventus) na Mario Balotelli, Keisuke Honda, Carlos Bacca na Kevin-Prince Boateng (Kwa upande wa AC Milan). Ninaamini hii ni fursa kubwa kwao na tunatajia mengi kwa wateja wetu siku za usoni.” Alihitimisha Bw. Geofrey.

No comments:

Post a Comment