Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, alipokuwa akizungumza kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu.
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Posta, Wilfred Miigo (kulia) na Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa shirika hilo, Joseph Ngowi, wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Meneja Masoko, David George (kushoto), Meneja Huduma za Barua, Fadya Zam (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Shughuli za Kimataifa, Elia Madules, wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza na kuchukua maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Baadhi ya waandishi wa habari na Maofisa wa shirika hilo, wakiwa kwenye mkutano huo jijini, Dar es Salaam leo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wakiwa kwenye mkutano huo, wakisikiliza na kuchukua maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo, akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, James Mahanga na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
KATIKA kuhakikisha kuwa Shirika la Posta Tanzania
linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za
Serikali ya Awamu ya Tano za kuleta maendeleo ya haraka kwa mwananchi na
kuifanya nchi yetu kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Shirika kuanzia
Jumanne litaanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa
mtumiwa (home/office delivery).
Huduma hii inayojulikana kama “Posta Mlangoni”itaanzia
katika baadhi ya kata za hapa jijini Dar es salaam, Arusha na Dodoma inaboresha
ile iliyokuwako tangu enzi za ukoloni ya masanduku yaliyoko Ofisi za Posta ambayo mtumiwa analazimika kufuata yeye
mwenyewe barua, vifurushi,taarifa au bidhaa alizotumiwa kupitia Ofisi za Posta.
Kwa hivi sasa yako masanduku 173,000 yaliyosimikwa katika Ofisi za Posta 172
zilizoko nchini.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais (TAMISEMI) tayari imeweka
miundombinu hiyo katika kata 8 za jiji la Arusha, kata 8 za manispaa ya Dodoma
na kata 32 kwajiji la Dar es Salaam.
Miundo mbinu hiyo ni mitaa kuwekewa nguzo zenye kuonyesha jina la mtaa,
nyumba zilizopo kwenye mtaa huo kuwekewa nambari za kiposta.
Mara baada ya kuanzisha huduma hii Jumanne ijayo hapa Dar
es Salaam, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2015/2016, awamu ya
pili itakayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 itahusu mikoa ya
Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mara, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani,
Manyara, Simiyu na Geita pamoja na Tanzania Visiwani (Unguja na Pemba). Awamu
ya tatu itatekelezwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 itakamilisha mikoa yote
iliyobaki ambayo ni Iringa, Mbeya, Songwe, Kigoma, Singida, Rukwa, Ruvuma,
Katavi na Njombe.
Huduma hii ni msukumo mpya wa ndani ya Shirika wa
kuhakikisha kuwa yanakuweko mabadiliko katika uendeshaji na utoaji wa huduma za
mawasiliano ya Posta nchini ili kukabiliana na kasi ya teknolojia, kukidhi
mahitaji ya soko, kuboresha maisha ya wananchi na kuifanya Tanzania kuwa kinara
wa huduma bora za mawasiliano
barani Afrika.
Kupitia huduma hii yamefanyika mabadiliko ya mifumo ya
uendeshaji katika baadhi ya Ofisi ili kuhakikisha kuwa uchambuzi wa barua
unafanyika kwa uhakika na haraka zaidi, anwani zinatambuliwa kwa urahisi na kuongeza
kasi katika kusafirisha na kusambaza barua, nyaraka, vifurushi na bidhaa za
wateja.
Aidha, katika kipindi hiki cha mpito ambapo hapo baadae
ndani ya kipindi cha miaka mitatu Shirika litasambaza huduma ya “POSTA
MLANGONI” nchi nzima, mfumo wa sasa wa anwani kupitia masanduku ya barua umeboreshwa ambapo wateja au wananchi wenye barua katika
masanduku yao watakuwa wanatumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu (sms) ili
kufuata barua zao hizo badala ya utaratibu wa sasa ambapo wanalazimika kusafiri
kwenda Posta bila ya taarifa ya kuwepo au kutokuwepo na barua katika masanduku
yao.
Huduma hii imeanzishwa sasa kutokana na jitihada mahususi
za Serikali kuweka Miundombinu ya Anwani za Makazi na Postikodi kupitia Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA) na wadau wengine.
Miundombinu hii ni pamoja na Barabara/Mtaa kupewa majina yanayosomeka
kwenye nguzo zilizosimikwa pamoja na nyumba kupewa namba kwa utaratibu
rahisi wa anwani pamoja na postikodi.
Postikodi au zip codekama inavyojulikana katika nchi
nyingine duniani ndiyo inayorahisisha
kumfikia mteja mahali alipo. Postikodi
ni alama za kiposta zenye namba zilizochanganywa na herufi ili kutambua sehemu
husika. Namba hizo zimeundwa kitaalamu kurahisisha
usambazaji wa barua ili mlengwa aweze kuipata barua yake. Nchini Tanzania, alama hizo zipo katika mfumo
wa namba pekee zenye tarakimu tano bila kuchanganya na herufi.
Kila Kata/Wadi katika nchi yetu imepewa Postikodi hiyo
yenye tarakimu hizo tano zenye kuwakilisha kata husika, wilaya iliyomo, mkoa na
kanda. Tanzania bara imegawanywa katika
kanda (6) za kipostikodi kuanzia 1-6, huku Zanzibar ikipewa (7). Hivyo kila Mtanzania anaweza kutambuliwa
makazi yake kwa kata anayoishi,
Barabara/Mtaa/Kijiji/Kitongoji na namba ya nyumba. Kwa hivi sasa Serikali
imekamilisha kanzidata (database) ya mfumo mzima wa anwani za makazi kwa nchi nzima na hivyo
kuwezesha anwani hizo kutambulika hadi ngazi ya kata/wadi hatimaye kuwezesha
kila mwananchi kuwa na anwani inayomtambulisha.
Anwani na Postikodi hizo ziko katika tovuti za Mamalaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) www.tcra.go.tz na Shirika la
Posta Tanzania (TPC) www.posta.co.tz.
Shirika la Posta Tanzania linatambua na kuzingatia kuwa
mifumo ya huduma za mawasiliano hususani haya ya Posta inabadilika kwa kasi
sana duniani. Kwa mfano, baadhi ya nchi zilizoendelea ziko katika tafiti na
majaribio ya mwishomwisho ya kuendesha huduma za Posta kwa kutumia mashini za
roboti au ndege zisizokuwa na rubani (drones), mfano Singapore na Uswizi.
Kwahiyo, pamoja na malengo mengine muhimu, malengo halisi
ya Shirika ya kuanzisha huduma ya “POSTA MLANGONI” ni kuhakikisha
kuwa watanzania wanafaidika na matunda ya huduma bora na za kisasa za
usambazaji na logistiki, huduma bora za kimtandao kama manunuzi mtandao (e –
shopping) kitaifa na kimataifa, kuwaongezea kasi katika matumizi ya sayansi na
teknolojia, kuwapunguzia umaskini na kwa ujumla kuwarahisishia uendeshaji wa
maisha yao ya kila siku ya kiuchumi na kijamii.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA POSTAMASTA MKUU
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
POSTA HOUSE, GHOROFA YA 12
7 MTAA WA GHANA
11300 DAR ES SALAAM
SIMU: 022 21133
94
068 48875 61
068 48879 66

No comments:
Post a Comment