Mamadou Sakho
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa kufeli ukaguzi wa madawa ya kulevya.
BBC radio 5 inasema kuwa Sakho alipatikana na dawa za kusisimua misuli baada ya mechi ya UEFA kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United.
Sakho aliyesajiliwa kwa pauni milioni 18 kutoka Paris St-Germain mwaka 2013 amecheza mechi 34 msimu huu ikiwemo mechi 10 katika ligi ya Yuropa.
Alifunga katika ushindi wa Liverpool wa 4-3 dhidi ya Borussia Dormund mnamo tarehe 14 mwezi Aprili na kufuzu katika nusu fainali ya kombe hilo.
Liverpool ambayo ni ya 7 katika jedwali la ligi ya Uingereza inaialika Newcastle siku ya Jumamosi.

No comments:
Post a Comment