TANGAZO


Monday, April 4, 2016

RC Makonda alipokabidhiwa Ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Sadiki

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhiwa Ofisi Mkuu wa Mkoa mpya wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wapili kushoto) na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecky Sadiki (watatu), jijini hivi karibuni. (Imeandaliwa na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, akijitambulisha wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Mofisa na Watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika hafla hiyo.
Mmoja wa Maofisa wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, akijitambulisha katika hafla hiyo.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) jijini hivi karibuni.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wapili kushoto) jijini hivi karibuni. Kulia ni Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na wa Ilala, Raymond Mushi. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumza katika hafla hiyo, ya kumkabidhi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto). Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kulia), ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akimkabidhi rasmi vitendea kazi vya mkoa, Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akimkabidhi Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Akimkabidhi nyaraka mbalimbali.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akisoma mambo mbalimbali anayopasa kukabidhiwa mkuu wa mkoa mpya.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akisaini hati ya makabidhiano. Kushoto ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akisaini hati ya makabidhiano. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando na katikati ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akimkabidhi vitendea kazi vyote Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati alipomkabidhi ofisi jijini hivi karibuni.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza wakati akitoa shukurani zake na kuelezea mwelekeo wake wa kiutendaji kwenye mkoa huo, mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wapili kushoto), jijini hivi karibuni.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), jijini hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB, Edmund Mkwawa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Chanika jijini hivi karibuni, wakati alipokabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadiki (hayupo pichani). Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa. Katikati ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki aliyemkabidhi rasmi ofisi hiyo.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya DCB.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa habari. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa blogu hii ya bayana, Kassim Mbarouk.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment