Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Balozi Simba aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo wizara hiyo.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi, Arcado Nchinga akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza
kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba (hayupo
pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Mkutano wa Baraza
hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es
Salaam.

No comments:
Post a Comment