TANGAZO


Monday, April 18, 2016

MBUNGE WA KINONDONI MHE. MAULID MTULIA AWAANDALIA MKUTANO ILI KUWASHUKURU NA KUSIKILIZA MATATIZO YAO WAPIGA KURA WAKE

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia (kulia), akisalimiana na kumkaribisha Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea, alipowasili katika mkutano wa kuwashukuru na kusikiliza kero za wananchi wa Kinondoni, ili kuziwasilisha Bungeni Mjini Dodoma katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwanachama mkongwe wa Chama cha Wananchi (CUF), Richard Hiza Tambwe, akihutubia katika mkutano huo. 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob, kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akihutubia katika mkutano huo, kuwaeleza wananchi wa Manispaa hiyo masuala mbalimbali ikiwemo bajeti ya manispaa hiyo.
Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akihutubia jana katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia, wa kuwashukuru na kusikiliza matatizo yao kwa ajili ya kuyapeleka Bungeni Mjini Dodoma.  
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakiwa katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni wa kuwashukuru na kusikiliza wapiga kura wake kuhusu masuala ya kuyawasilisha Bungeni Mjini Dodoma.
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakiwa katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni wa kuwashukuru na kuwasikiliza matatizo yao kwa ajili ya kuyawasilisha Bungeni Mjini Dodoma.
Wananchi wa Kinondoni wakimsikiliza Mbunge wao, Maulid Mtulia alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru na kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuziwasilisha Bungeni Mjini Dodoma. 
Wananchi wa Kinondoni wakifurahia hotuba zilizokuwa zikitolewa na Mbunge wao pamoja na viongozi wa Ukawa wakati wa mkutano huo wa kuwashukuru na kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuziwasilisha Bungeni Mjini Dodoma Magomeni jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia (kulia), akielezwa jambo na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya wakati wa mkutano wa mbunge huyo na wananchi wa jimbo lake katika kuwashukuru na kusikiliza kero zao ili kuziwasilisha bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea akizungumza na wananchi wa jimbo lake Kinondoni, wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Maulid Mtulia kuwashukuru na kusikiliza kero zao ili kuziwalisha bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwashukuru na kusikiliza kero zao ambazo ataziwakilisha katika kikao cha Bunge Mjini Dodoma.
Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kinondoni wakimsikiliza Mbunge wao, Maulid Mtulia alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru na kusikiliza kero zao ili kuziwakilisha Bungeni Mjini Dodoma. 

No comments:

Post a Comment