Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athuman
Na Immaculate Makilika –MAELEZO
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa
Polisi Diwani Athumani amesema hadi kufikia sasa zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao, katika hatua ya kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda.
“Baada
ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kufanya uhakiki wa silaha zake hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo
viongozi mbalimbali waliopo Serikalini, Viongozi wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali,
wafanyabiashara na wabunge wamejitokeza kuhakiki silaha zao, na wengine wameonesha nia ya
kufanya hivyo, hata hivyo tusingependa
kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama” amesema Kamishna wa Polisi Athumani
Athumani
amesema kuwa, lengo la kufanya uhakiki wa silaha ni pamoja na kuboresha hali ya
usalama na kuwajua watumiaji, kuwatambua tena wamiliki wa silaha pamoja na kuwa
wanawatambua isipokuwa zinaweza kutokea
sababu mbalimbali zitakazofanya wasiendelee kumiliki silaha hizo ikiwemo vifo
na ulemavu na kusema kuwa wangependa kufahamu taarifa za namna hiyo,
ameongeza kuwa zoezi hili sasa ni la
nchi nzima si kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kama ilivyokuwa hapo awali.
Aidha,
wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wanaweza
kuhakiki silaha zao katika vituo vya Osterbay Polisi, Temeke Chang’ombe Polisi na
Ilala central Polisi, ambapo wanatakiwa kwenda na kitabu (firearm licence book), picha ndogo nne za mhusika, pamoja na anwani sahihi ya mahali anapoishi mhusika.
Vilevile,
amewataka viongozi mbalimbali na wananchi wanaomiliki silaha kujitokeza kwa
ajili ya kufanya uhakiki wa silaha zao huku akisisitiza kwa wakazi wa Mkoa wa
Dar es salaam, wanaweza kuonana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
salaam, Simon Sirro na kwa wakazi wa Mikoani waonanae na makamanda wa polisi wa
Mikoa yao kwa ajili ya kupewa msaada na maelekezo zaidi ya taratibu za kufuata ili waweze kufanya uhakiki wa silaha zao.
No comments:
Post a Comment