TANGAZO


Saturday, March 26, 2016

Mshukiwa wa Paris Abdeslam akataa kuongea

Image captionMashukiwa wa Paris Abdeslam
Mshukiwa wa shambulizi la mjini Paris Salah Abdeslam amekataa kuzungumza alipoulizwa kuhusu shambulizi la mjini Brussels ,kulingana na waendesha mashtaka wa Ubelgiji.
Wanasema kwamba Abdeslam aliyekamatwa wiki iliopita mjini Brussels na ambaye amekuwa akishirikiana nao ameamua kutimiza ''haki yake ya kunyamaza'' na kutojibu lolote alipohojiwa baada ya mashambulizi ya Jumanne.
Alikamatwa siku chache kabla ya shambulizi hilo ambapo takriban watu 31 waliuawa.
Watu 12 walikamatwa siku ya Alhamisi na Ijumaa katika mataifa matatu.
Sita kati yao walikamatwa nchini Ubelgiji siku ya Alhamisi na wengine watatu wakikamatwa siku ya Ijumaa ijapokuwa washukiwa kadhaa baadaye waliachiliwa.
Image copyrightAP
Image captionSalah Abdeslam akikamatwa na maafisa wa Polisi
Wakati huohuo maafisa wa Ubelgiji wamemtaja mlipuaji wa pili wa kujitolea muhanga mjini Brussels kama Najim Laachraoui,na kusema chembechembe zake za visaba vya DNA pia vilipatikana katika eneo la shambulio la Paris mnamo mwezo Novemba.
Kundi la wapiganaji wa IS tayari limekiri kutekeleza mashambulizi yote ya Brussels na Paris.

No comments:

Post a Comment