TANGAZO


Thursday, March 24, 2016

Mshukiwa wa Brussels aliunda mabomu ya Paris

Mashambulio Watu wengi walijeruhiwa kwenye mashambulio hayo

Maafisa wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu.
Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa Paris.
Hajatambuliwa rasmi hata hivyo.
Watu 34 walifariki na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek.
Najim
Najim Laachraoui
Kundi la Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo.
Msako mkubwa unaendelea kumsaka mshambuliaji ambaye hajatambuliwa na ambaye anaaminika kutoroka.
Washambuliaji wawili wametambuliwa kama ndugu Khalid na Brahim el-Bakraoui.

No comments:

Post a Comment