TANGAZO


Tuesday, March 22, 2016

ISAYA CHACHA WA CHADEMA (Ukawa) ASHINDA UMEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM LEO


Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Yenga  Yusuph alipokuwa akiomba kura kwa wajumbe walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Anitha Jonas-Maelezo)


Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowasa akimpongeza mshindi wa nafasi ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia chama hicho chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mhe. Isaya Chacha mara baada ya kutangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Viti Maalum  Kinondoni  kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Suzan Lyimo (kushoto) pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee (CHADEMA) wakifuatilia zoezi la Upigaji kura wa kumchagua  wa Meya leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Agustine Mahiga akizungumza na aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yenga Yusuph.

Baadhi ya wapiga kura waliohudhuria uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Leo 22/03/2016 wakifuatilia uchaguzi huo.

Baadhi ya Maofisa kutoka  Ofisi za  Jiji Dar es Salaam wakifuatilia Uchaguzi wa Meya uliyofanyika leo (kwa kwanza kulia) ni  Afisa Sheria Mkuu  Jumanne Mtinangi.

Baadhi ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya wa Jiji leo Dar es Salaam (Kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Kaluwa.

No comments:

Post a Comment