FDC kimetaka vikosi vya usalama kuacha kuzingira sio tu nyumba na mshika bendera wake lakini pia na ofisi zao.
Mkuu wa chama hicho, Meja Jerali Mustaafu Mugisha Muntu, mbele ya waandishi habari katika makao ya chama hicho mtaa wa Najanankubi mjini Kampala ametaka serikali itoe mzingiro katika nyumba ya Dkt Kizza Besigye.
FDC inadai kuwa wafuasi wake zaidi ya 300 baadhi wakiwa mawakala wamekuwa wakikamatwa kiholela nchini kote.
Aidha kinashuku matokeo ya uchaguzi ambayo yalitangazwa na tume ya uchaguzi iliompa ushindi Museveni, huku Meja Jenerali Mugisha akitoa sababu ya kuunda kwa tume hiyo.
Hata hivyo amepinga wazo la kutumia mabavu kufikia malengo yao akisema kuwa hiyo sio njia yao.


No comments:
Post a Comment