TANGAZO


Wednesday, February 24, 2016

Ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea  na menejimenti ya  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa   ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake. (Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo) 
Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)Arch.Elius Mwakalinga akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (hayupo katika picha) alipotembelea ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa  ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake. 
Wafanyakazi wa   Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika  ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo. 
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo katika picha) Mamilo  katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mhandisi Julius Mamilo (kulia) wakati ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment