Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hiyo dhidi ya JKT Ruvu Stars Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 4-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mbuyu Twite wa Yanga akiruka baada ya golikipa wa JKT Ruvu kuudaka mpira wakati wa mchezo huo.
Mbuyu Twite wa Yanga akiruka baada ya golikipa wa JKT Ruvu kuudaka mpira wakati wa mchezo huo.
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga 1 na JKT Ruvu 0.
Mbuyu Twite akishangilia bao la pili la Yanga.
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga 2 na JKT Ruvu 0.
Donald Ngoma wa Yanga kikimbia na mpira.
Donald Ngoma wa Yanga kikimbia na mpira, huku akifuatwa na wachezaji wa JKT Ruvu.
Deus Kaseke wa Yanga akiwania mpira na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu.
Paul Nonga wa Yanga akiwania mpira na Madenge Ramadhan wa JKT Ruvu.
Deus Kaseke wa Yanga akiudhibiti mpira huku Madenge Ramadhan wa JKT Ruvu, akijaribu kuuondoa miguuni mwake.
Haruna Niyonzima wa Yanga akiudhibiti mpira.
Haruna Niyonzima wa Yanga akiwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.
Donald Ngoma akiudhibiti mpira huku akifuatwa na mchezaji wa JKT Ruvu.
Donald Ngoma wa Yanga, akipiga mpira huku akifuatwa na Nurdin Mohamed.
Donald Ngoma wa Yanga, akipongezwa na mchezaji mwenzake Paul Nonga (26) baada ya kuifungia timu yao hiyo bao la 3 kati ya 4 - 0, iliyoshinda timu hiyo dhidi ya JKT Ruvu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Donald Ngoma (11) baada ya kuifungia timu yao hiyo bao la 3 kati ya 4 - 0, iliyoshinda timu hiyo dhidi ya JKT Ruvu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

No comments:
Post a Comment