TANGAZO


Wednesday, February 24, 2016

Wenger aikosoa safu yake ya mashambulizi

Image copyrightReuters
Image captionWenger
Kilabu ya Barcelona imefuzu asilimia 95 katika michuano ya robo fainali ya kombe la vilabu bingwa barani Ulaya ,mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema baada ya kilabu yake kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa hao wa Uhispania.
Raia huyo wa Ufaransa aliilaumu safu yake ya mashambulizi kwa kushindwa kufunga na kukosa kujua cha kufanya wakati wa mechi hiyo.
Alex Oxlaide Chamberlain na Olivier Giroud walikosa nafasi za wazi kwa upande wa Arsenal kabla ya Barcelona kufunga bao lao la kwanza
Image copyrightReuters
Image captionGiroud
''Vile tulivyomaliza nafasi zetu ilikuwa matatizo.Nilihisi katika kipindi cha mwisho tulikosa kiufanya kitu muhimu,''alisema Wenger.
''Barcelona wamefuzu asilimia 95,lakini tunataka kwenda huko kucheza.Hatutakwenda huko kuchezewa,''aliongezea.

No comments:

Post a Comment