TANGAZO


Tuesday, February 9, 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Tanzania Investment Bank (TIB) Peter Noni akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Omary Issa akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Ajira Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Beng’I .M. Issa (NEEC) akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa, akikabidhi kitabu cha Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Beng’I .M. Issa wakati akifungua mkutano wa Baraza la Uwezeshaji uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Tanzania Investment Bank (TIB) Peter Noni ikiwa ni shukrani kwa kufadhili katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe.Kassim Majaliwa, akimsikiliza  Afisa Mauzo na Masoko  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Rhobi Wambura wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe.Kassim Majaliwa, (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Omary Issa wakati wakizungumza baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Uwezeshaji kuhusu Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Mwalimu J K Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Ajira Mhe.Jenista Mhagama. 
Waziri Mkuu wa Tanzania  Mhe.Kassim Majaliwa, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Baraza la Uwezeshaji. (Picha zote na Raymond Mushumbusi-Maelezo)

Na lilian Lundo-Maelezo
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo amezindua mwongozo wa utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika mkutano wa wadau wa uwezeshaji kiuchumi.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) umeshirikisha wadau mbalimbali kama vile Tanzania Investment Bank(TIB), Tanzania Poster Bank (TPB), UTT Microfinance, World Vision, CRDB, National Housing Cooperation (NHC), PSPF, GEPF ambao wanachangia katika kuendeleza uchumi wa mwananchi.

Katika hotuba yake Mhe. Majaliwa alisema kuwa utekelezaji wa kila siku wa Serikali unamlenga mwananchi wa hali ya chini ili kumuinua kiuchumi. Hivyo amewataka wadau wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kusaidiana na Serikali katika kuinua uchumi wa mwananchi wa hali ya chini.

“Katika kikao hiki angalieni maeneo ambayo yanalenga matokeo ya haraka kama vile kilimo, uvuvi, viwanda, ufugaji, biashara, utalii na madini ili kumwezesha mwananchi wa chini kujikwamua kimaisha na kuinua uchumi wake,” alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha,Mhe. Majaliwa aliwataka wadau wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kushirikisha wananchi katika kujenga uchumi na kuwasaidia kupata mitaji kwa gharama nafuu ambayo itazingatia riba itakayokuwa rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuirudisha kutokana na biashara anayoifanya.

Mhe. Majaliwa ameitaka NEEC kuangalia namna gani mtaala wa ujasiriamali utaanza kufundishwa kuanzia elimu ya msingi mpaka vyuo vikuu ili kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana ilikuwawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa na Serikali au mashirika binafsi.

Dira ya Maendeleo ya Taifa imeainisha kuwa ifikapo mwaka 2025 sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania iwe inamilikiwa na Watanzania wenyewe, hivyo shughuli zote za uwezeshaji zinatakiwa zifanywe kwa ushiriki wa wadau wote ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na fursa sawa za biashara ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment