Mtangazaji wa Luninga na Redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) ambaye pia ni balozi wa kampuni hiyo kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akipiga nambari ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya pili ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wakiuatilia tukio hilo kwa makini kulia ni Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Damien Leo (kulia) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (katikati).
Meneja wa Masoko wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Leo (katikati) akiuatilia kwa makini mazungumzo kwa njia ya simu baina ya mshindi wa droo ya pili ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mtangazaji wa Luninga na Redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (kushoto), ambaye pia ni balozi wa kampuni hiyo kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo. Akinakili taarifa hizo katikati ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Februari 12, 2016
WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujishindia safari ya kwenda kutazama ‘Live’ moja ya mechi za ligi ya Ujerumani inayotolewa na kampuni ya StarTimes Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchezeshwaji wa droo ya pili ya promosheni hiyo, Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Damien Leo amebainisha kuwa tayari mshindi wa kwanza amekwishapatikana na leo hii kama mlivyoshuhudia wa pili nae tumemtangaza.
“Dhumuni kubwa la kufanya promosheni hii ni kuwakumbusha wateja wetu kuwa StarTimes imejizatiti katika kuboresha maudhui ya chaneli na vipindi vinavyopatikana katika ving’amuzi vyake. Kama ukifuatilia kwa ukaribu tumekuwa tukifanya maboresho mara kwa mara ili kukidhi haja ya watazamaji wa kila rika. Kwa mwaka uliopita tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kuongeza chaneli na vipindi vya michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, kikapu, tenesi, riadha, kuogelea, mbio za magari, pikipiki na kadhalika.” Alisema Bw. Leo
“Hivyo basi kwa wao kulipia vifurushi vya mwisho wa mwezi au kujiunga na huduma zetu, licha ya kuwa katika nafasi ya kushinda safari hii bali pia wataweza kujionea mazuri tuliyonayo. Ningependa kutoa wito kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla kujijengea utamaduni wa kujaribu vitu tofauti,” alisema na kumalizia Bw. Leo, “Tusiwe na mazoea ya kutazama chaneli na vipindi vya nyumbani pekee tu, tujaribu na kwa upande wa wenzetu wanafanya nini. Nina amini vipo vitu vingi vizuri vya kutazama, kujifunza na kuvifanya huku nyumbani na kuleta manufaa kwa jamii yetu.”
Katika droo hiyo ya pili iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Bw. Johannes Maluli (53), mkazi wa Vingunguti na kujishughulisha na udereva, alibahatika kuwa mshindi baada ya namba ya smati kadi yake ya king’amuzi kuibuka miongoni mwa moja wapo ya yenye bahati.
Akielezea juu ya ushindi huo kwa njia ya simu Bw. Maluli alisema kuwa amepokea habari hiyo kwa furaha kubwa na kuishukuru kampuni ya StarTimes kwa kuja na promosheni hiyo kubwa na aina yake kwa wateja.
“Nashukuru sana kupokea habari hii njema na pia ningependa kuwapongeza waandaji kwani hili jambo kubwa sana wanalolifanya kwa sisi wateja wao. Ni kampuni chache zinafanya hivi na hata kama wakifanya huwa wanatoa zawadi za kawaida lakini hii ni tofauti. Sitoamini macho yangu mpaka pale nitakapoigusa ardhi ya Ujerumani, hapo sasa ndio nitaamini kuwa StarTimes kuwa walikuwa hawatanii. Ningependa kuwataka wateja wenzangu na watanzania washiriki katika promosheni hii kwani ni kweli na si ubabaishaji na tena ukizingatia vigezo na masharti ni nafuu kabisa.” Alihitimisha Bw. Maluli
Mshindi huyo wa pili wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Mambo ambacho ni shilingi 12,000 katika king’amuzi cha antenna. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.




No comments:
Post a Comment