Askari wa usalama wa Israili, wamewapiga risasi na kuwauwa vijana watatu wa Palestina katika ufukwe wa Magharibu unaokaliwa na taifa hilo la kiyahudi.
Jeshi la Israil linasema wawili kati yao waliwashambulia kwa mawe, askari waliokuwa wanapiga doria, na walitumia bastola.

Mpalestina mwengine aliuwawa baada, inavyodaiwa, kujaribu kumpiga kisu polisi wa mpakani karibu na Jerusalem na Bethlehem.
Hakuna Mu-Israili aliyeumia katika tukio hilo.


No comments:
Post a Comment