TANGAZO


Saturday, February 27, 2016

Wanajeshi 100 kupelekwa nchini Burundi

Image copyrightAP
Image captionJacob Zuma
Umoja wa Afrika umetangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki za kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini Burundi.
Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza ameunga mkono mpango huo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika ziara ya siku mbili wiki hii.
Image copyrightPresidency ZA
Image captionJazob Zuma
Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi wawili wa upinzani ambao wamesalia nchini humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi Aprili baada ya Nkurunziza kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment