TANGAZO


Sunday, February 7, 2016

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wafanya sherehe ya kuwaaga wastaafu, mwaka 2015 Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakivutana kwa kamba wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Timu za Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), za Post Cargo (kulia) na EMS, wakivutana kwa kamba wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. 
Timu za Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), za Post Cargo (kulia) na ikivutwa na EMS, wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo.  
Ofisa Mkuu Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Abdi Mchonga, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe hizo.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakijadili jambo, wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. 
Timu ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), ya EMS, wakijiandaa kuvutana na wenzao wa PostCargo, wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. 
Timu za Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), za Post Cargo (kulia) na ikivutana na EMS, wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. 
Wafuta kamba wa timu Post Cargo wakishangilia baada ya kuwavuta wenzao wa EMS, wakati wa kusherehekea kuwaaga wastaafu, kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. 

Juu na chini wafanyakazi wakifanya mahojiano na waandishi wa habari, wakati wa sherehe hizo. 

Wafanyakazi wakishindana kukimbia wakati wa sherehe hizo. 
Wafanyakazi wakishindana kukimbia kwa mbio za magunia, wakati wa sherehe hizo.  
Wafanyakazi wakishindana kukimbia na mayai kwenye vijiko mdomoni, wakati wa sherehe hizo.  
 Washindi wakiwania koni ya kuwa wa kwanza wakati wakishindana kukimbia na mayai kwenye vijiko mdomoni, katika sherehe hizo.  
Wafanyakazi wakijiburudisha na kuangalia michezo ilivyokuwa ikiendelea. 
Wafanyakazi wakibadilishana mawazo wakati michezo ikiendelea.  
Wafanyakazi wakifuatilia michezo ilivyokuwa ikiendelea.  
Wafanyakazi wakifurahia michezo hiyo wakati ikiendelea.  
Wafanyakazi wakikimbiza kuku katika kusherehekea hafla hiyo.  
Wafanyakazi wakifuatilia michezo na shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika hafla hiyo. 
Wafanyakazi wakifurahia michezo ilivyokuwa ikiendelea.  
Mmoja wa washindi wa shindano la kufukuza kuku akiwa amemshikilia kuku aliyemshika katika shindano hilo. 
Mmoja wa washindi wa shindano la kufukuza kuku akimrukia kuku huyo katika shindano hilo.  
Mshindi wa shindano la kufukuza kuku akiwa amemshilia kuku wake baada ya kumkamata. 

Irene Mtenga (BBTC)
SHIRIKA la Posta Tanzania wamefanya sherehe za kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, zilizoandamana na tukio la kuwaaga wastaafu wa kampuni hiyo na michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Ufukwe wa Msasani jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkuu Mwandamizi wa shirika hilo, Abdi Mchonga, alisema wanafurahi kujumuika pamoja na kuwaaga wafanyakazi wenzao kwa kutumikia kwa uaminifu shirika hilo.


"Tunafurahi sana kujumuika pamoja, kama ndugu na kusherehekea pamoja tafrija hii, japo tutakuwa na huzuni kidogo kwa wenzetu tunaowaaga," alisema.


Alisema kuwa, wamewaalika wadau wa biashara katika sherehe hiyo kwa matarajio ya kubadilishana mawazo ili kupata njia mpya katika kuboresha  huduma zao na kuwaweka jamii wanayoitumikia karibu zaidi.


Grace Kisanga ambaye ni mmoja wa wastaafu ndani ya shirika hilo, alilolitumikia shirika hilo kwa muda wa miaka 38, alisema anayofuraha kubwa kwani, akiwa ndani ya shirika hilo aliweza kutoa huduma kwa jamii inayomzunguka.


Wafanyakazi hao walicheza michezo mbalimbali, ikiwemo riadha, kukimbiza kuku, mbio za gunia, kukimbia na mayai na michezo mingine mingi kwa ajili ya kujenga mwili.


Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, Mbarouk Sasilo, alisema kuwa, sherehe hiyo imewafanya kuwa pamoja na kufurahi kama familia.


"Kwanza tunaitangaza huduma yetu kwa jamii ili wazidi kuliunga mkono Shirika la Posta na pia, inatufanya kuwa karibu zaidi na wakuu wetu wa 


vitengo na kubadilishana mawazo ili kukuza huduma zetu kote nchini," alisema Sasilo.

No comments:

Post a Comment