TANGAZO


Monday, February 8, 2016

Wachezaji wa DR Congo walakiwa kishujaa

Congo

Image captionDR Congo walilaza Mali 3-0 Jumapili
Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelakiwa kwa shangwe na nderemo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.
Hii ni baada yao kutwaa ubingwa wa Afrika katika michuano ya wachezaji wanaochezaji ligi za nyumbani (CHAN).
Raia wa nchi hiyo walijitokeza katika barabara za miji kuwakaribisha wachezaji hao.
Michuano ya mwaka huu iliandaliwa nchini Rwanda.
DR Congo walitwaa ubingwa kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali.
CHAN
Image captionMichuano ijayo itaandaliwa nchini Kenya
Taifa hilo ndilo la pekee kutwaa ubingwa wa CHAN mara mbili.

No comments:

Post a Comment