Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Tamasha la Pasaka litakalofanyika mikoani kuanzia Machi 26 mwaka huu. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Tamasha la Pasaka
litakalofanyika mikoani kuanzia Machi 26 mwaka huu.
Irene Mtenga (BBTC)
TAMASHA la Pasaka mwaka huu litafanyika katika mikoa tofauti nchini na kubeba taswira tofauti na matamasha yaliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema kuwa wamefikia uwamuzi wa kuandaa Tamasha hilo mikoani ili kuwapa fursa watu wa mikoani kuhudhuria tamasha hilo.
"Mara nyingi tumekua tukiandaa Tamasha hili, Dar es Salaam pekee na watu wa mikoani wanakosa fursa ya kuhudhuria kutokana na wengine kuwa na uwezo mdogo kiuchumi, hivyo safari hii ni zamu yao," alisema.
Tamasha litaanza katika mikoa ya Geita Jumamosi ya Pasaka tarehe 26, Mwanza Jumapili na Kahama Machi 28, baadae itafuata mikoa mingine nchi nzima.
Msama alisema kuwa Tamasha hilo litabeba sura mpya mwaka huu kwa kuwapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi zaidi na wa nchi za nje kwa idadi ndogo.
Tamasha ambalo limebeba kauli mbiu ya "Umoja na Upendo hudumisha Amani ya Nchi" linatarajiwa kuwa na waimbaji mashuhuri nchi kwa upande wa nyimbo za injili akiwemo Bonifasi Mwaitege na Rose Muhando wakisindikizwa na wasanii wengine wa injili nchini.
Aidha Msama alisema kuwa wanaishukuru Baraza la Sanaa Tanzania BASATA, kwa kutoa kibali cha kuandaa tamasha hilo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.
"Tunajali na kuwapenda Watanzania wenzetu kama ambavyo kauli mbiu inavyosema, Tanzania yote ni wa moja tuzidi kushirikiana kufanikisha hilo," alisema Msama.



No comments:
Post a Comment